Kama sikosei Nsajigwa Shadrack alizaliwa mwaka 1981,Rungwe Mbeya...
Elimu ya Sekondari alisoma Sangu Secondary Mbeya...
Mpira alianza kucheza tangu akiwa mdogo(chandimu)....
Alianza kuwika zaidi akiwa na timu ya Mount Rungwe ya Tukuyu,Mbeya ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la 3 mkoa wa Mbeya enzi hizo...
Aliichezea Mount Rungwe mpaka mwaka 1999 ambapo mwaka huohuo alijiunga na timu ya Kyela United ya Kyela,Mbeya iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la 3 ngazi ya mkoa wa Mbeya.....Nakumbuka alihamia Kyela United akiwa na mchezaji aitwaye KAISI ambaye ni rafiki yake na alikuwa na kipaji cha hali ya juu(sijui yuko wapi Kaisi)....Akiwa Mount Rungwe na Kyela United alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Nsaji ama Jigwa...
Baada ya kutoka Kyela United alijiunga na Prisons ya Mbeya ambako hakukaa muda mrefu sana akahamia(yeye na swahiba wake Ivo Mapunda) timu ya Moro United ya Morogoro ambako alikaa msimu mmoja mpaka mwaka 2005 yeye na Ivo walipojiunga rasmi na Yanga na tangu wakati huo(mwaka 2005) hajahama Yanga licha ya misukosuko aliyoipata mara kwa mara akiwa na Yanga......
Kwa uchache naweza kusema huu ndio wasifu/historia ya Nsajigwa Shadrack