Kama unataka kuomba as a fresh student then subiri.Lakini ningekushauri utafute chuo kingine cha kusoma.Utakuja kujua kuwa hiki chuo hakitambuliki na elimu yako ni form six tu.Najua wengi hamjui sana undani wa elimu hii hasa kwa hapa kwetu.Ukiingia utakuja jua kuwa ulipoteza muda ni bora ungejiunga na chuo kingine kusoma mambo ambayo unaweza pia kujiajiri.Elimu hii haitakusaidia kujiajiri.Sikukatishi tamaa ila utamu wa ngoma ingia ucheze.Ushauri wangu ni huo.Kuna kera huko usisikie.Lakini nimekushauri tu uamuzi wa mwisho ni wako maana inawezekana kuna mtu unamjua anafanya kazi huko na hakutaka kukueleza ukweli wa mauza uza yaliyopo huko.