NACTE Msikwepe Majukumu

TUTUO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
3,250
Reaction score
2,036
Niende moja kwa moja kwenye hoja,

Enyi watu wa NACTE specifically mnaoshughurika na Award Verification System (AVN) ,ni wiki ya pili sasa tangu niombe hyo AVN lakini cha ajabu majibu sipewi through email na namba ya simu niliyowapa bali najibiwa na system tu inayosema subiri after 72hrs zikiisha inajirudia tena, mnanambia hamna information zangu nikiambie chuo nilichosoma kitume really?

Si ni nyie muwasiliane nao maana kipo chini yenu mi nilishaleta taarifa zangu zote kwenu na mkanipa na evaluation letter leo mnasema hamna taarifa zangu sasa hyo evaluation mlifanyaje? Mnatukwamisha sana watu wa diploma wakati mkijua muda wa kuomba vyuo unaisha na hatuwezi kusubmit maombi bila ya hiyo namba .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pathetic.

Hiyo service ni bure au unalipia directly kwao tena?
 
Wameona ila fuata maelekezo yaliyopo kwenye system yatakusaidia sana
 
Hamna maelezo ya maana zaidi ya system kukwambia subiri 72hrs maana hawapokei simu wala kujibu email.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hilo la kusubiri tayari ni la maana acha kuchokonoa chokonoa ili waifikie yako sasa we hujaona ile warning pale chini? Fuata maelekezo dogo.
 
Wewe ndio wa kushughulika na chuo ulichosoma kipeleke taarifa zako.. Sasa hao NACTE wataota kama kuna mwanafunzi anaitwa tutuo ambaye chuo chake hakijaleta matokeo yake?
 
NACTE ni jipu lililopewa majukumu mazito bila kujipanga na kujua wanahitaji kuhudumia wanafunzi. Nilipita hapo nilikuta umati wa watoto nikadhani Tb joshua anaponya vijana kwenye foleni

Tatizo la wabongo si walijua hata siku ya mwisho tutachelewa tu kwanye ufalme wa mbingu maana twajifanya busy for nothing. Hao ni wanaopenda dakika za mwisho wangine hatukuenda hata kufoleni pale na huduma ikawa murua. Sasa hapa jipu ni nani kama sio mwanafunzi mwenyewe.
 
Wewe ndio wa kushughulika na chuo ulichosoma kipeleke taarifa zako.. Sasa hao NACTE wataota kama kuna mwanafunzi anaitwa tutuo ambaye chuo chake hakijaleta matokeo yake?
Wewe Umeomba hyo avn au unakurupuka tu? Unapoomba una submit vyeti vyako na unajaza details zote za uliposoma sasa why mimi tena niende tena chuo nilichosoma au unahisi waombaji wote wanakaa Dar? Chuo nilichosoma kipo chini yao kwanini wao wasiwaulize chuo kwanini hakijapeleka taarifa za wahitimu wake? Kama nawe uko hapo nacte wafikishie ujumbe wenzio.
 
Hilo la kusubiri tayari ni la maana acha kuchokonoa chokonoa ili waifikie yako sasa we hujaona ile warning pale chini? Fuata maelekezo dogo.
Ndugu hayo masaa 72 yakiisha system inaji update tena usubiri muda huo huo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…