Ni elimu ya muhimu sana kwa watoto wetu wa sasa uwe umemnunulia simu ama la. Nasema hivyo kwa sababu gani wewe kama mzazi unawea kuwa hujamnunulia kwa sababu mbili. Moja ni kwa sababu huna uwezo na ya pili huoni umuhimu wa mtoto wako kuwa nao vifaa hivi kwa wakati huo.
Uzuri wa kumpa elimu hiyo ni kwavile shule wanaweza kuwa na vifaa hivi na wanatumia, marafiki zao wanawea kuwa nao na hata kuna sehemu hizi za kuperuzi maarufu kama cybercafé.
Mtoto akiwa amepata elimu hii itamsaidia hata akikutana na challenge yoyote kama wale watu wazima wanao kaa mitandaoni na kupenda kuchat na watoto wadogo na kuwadanganya wakutane nao, kuwaongelesha mambo ya mapenzi na yasiyo na maadili, kuwaambia wawatumie picha cha utupu ama hata wao kuwatukia picha ama hata kuwaonyesha miili yao wakiwa bila nguo moja kwa moja kutumia video calls, mtoto akishapata elimu hii na umwambie ikiyokea jambo lolote kati ya hayo na lingine lolote ampe taarifa mzazi mlezi ama hata mwalimu.
Na pia ajaribu kuto chat na mtu yoyote usie mjua mtandaoni. Itazuia kwa kiasi kikubwa kumlinda mwanao.