Wapendwa habarini za saa hizi.
Naombeni msaada wa ufahamu. Nataka kujua kuwa mwanafunzi anapokuwa nyumbani anasubiria matokeo ya fom 4 huwa hawi na kinga ya mwanafunzi tena?
Mi binafsi sipendi wadogo zangu wa kike waje wapate tabu kama ninavyoona wanawake ambao wameolewa wakiwa hawana ajira yoyote ya kuwapa hata uwezo wa kujikimu wenyewe. Hata mahitaji yao binafsi mfano hata mafuta mpaka amuombe mumewe. Ndio wanabadilishwa majina na kuitwa "magolikipa". Sikupenda waje wawe hivyo. Ukweli nlijitoa kuwapa kila walilohitaji; nilipambana na kujinyima kadri ya mahitaji yao na MUNGU akajalia mmoja akafanikiwa kuhitimu vizuri na kupata digrii yake.
Mwingine akaluzi mwanzoni. Alifeli form 4. Nikakaa naye chini nikamuuliza kulikoni, akaniambia kaka nilikuwa sipati muda wa kusoma kwa ajili ya kazi kijijini. Nkamwambia, sasa nkusaidieje mdogo wangu, japo umefeli we bado ni mdogo wangu. Akaniambia kaka naomba nipeleke shule tena kwa sasa sitakuangusha.
Hapo alikua na umri wa miaka kumi na saba. Nikamchukua na kumpeleka shule nkiwa na lengo la kumrudisha kidato cha pili lakini tulipofika hapo shuleni nakumbuka wanafunzi walikua break ya saa nne. Mkuu akamuuliza binti utaweza kidato cha pili? Binti akamjibu nitaweza mkuu, akamuita mtoto 1 wa kidato cha pili kamwambia ampokee mwenzake na wazunguke mazingira ya shule dk 5 alafu warudi.
Binti kurudi akanambia, kaka mi sitawezana na form 2 kwani kuna vitu vingi mimi sivijui; naomba nianze fom 1. Nikashauriana na mwalimu kisha wazazi mwisho tukaridhia wote, binti akapambana MUNGU akamjalia mwaka jana akahitimu.
Si akarudi kijijini akiwa anasubiria matokeo, akakutana na kidume kikamdanganya, mara ujauzito. Ila mi sijui mambo ya ujauzito, mi nasubiria matokeo. Mara matokeo yakaja kapata division 3, nikasema asante MUNGU, nafuu!
Namuuliza nikutaftie shule ye akaniambia hapana kaka, mi nataka chuo. Namuomba kabisa mdogowangu nenda 5,6 anakataa katukatu, kumbe anajijua amebeba nini tumboni.
Mpaka mwezi wa 5 yule kidume akamtorosha nyumbani kijijini. Wazazi na ndugu na mjirani wakamtafuta bila mafanikio. Siku ya 2 baba nkwamwambia akaripoti police; siku ya 3 na 4 ikaisha ikabidi nami niingilie kati; nami nikaenda kwa RPC, RPC akatoa amri OCD wa wilaya aharakishe upatikanaji wa mtoto. Ndipo akatoa amri nami nkapewa namba ya binti nikpewa mpelelez 1, tukamtrack siku ya 7 tukamkuta kidume mwenyewe. Ni kijana wa jirani na alihisiwa tangu mwanzo lakini alikuwa hataki kukubali.
Akawekwa ndani usiku, asubuhi yake binti akatokea nikafungua kesi. Binti kwenda kupimwa akakutwa na ujauzito wa miezi 5. Kesi imeendelea leo hii naambiwa kuwa eti tukaelewane nyumbani sababu eti kesi itakuja kuisha kwa aibu sababu binti hakuwa mwanafunzi, na hata mwalimu akienda kutoa ushahidi atasema binti alikua sio mwanafunzi wakati anaenda kupata ujauzito.
Sasa nmeshindwa kujua ukomo wa mwanafunzi ni upi.
Naombeni msaada nielewe hilo. Ndiyo ndoto za kumsaidia mdogo wangu zimeishia hapo au?