Mkuu unisamehe mwacha Mwl apumuzike huko,usipoteze muda wako na misemo ya Mwalimu.
Alianza vizuri akisema katika kimombo:It can be done play your part,kuhusu maadui watatu yaani Ujinga,Maradhi,Umaskini.
Na hiyo ndio miaka michache ya mwanzo,ambako tulikuwa tuna misingi ya kufanya kazi kama alivyotuachia mkoloni tukiwajibika kwa wananchi period.
Lakini mara baada ya kuanzisha AFRICANIZATION akiwandoa wazungu,na wageni kwenye nafasi zao na kuwaajiri wana Tanu wengi wao wasio na sifa za kazi kwa upendeleo, ndio magonjwa ya rushwa,uzembe,yalipoibuka kwa nguvu.
Ili kuzima mtafaruku ulioukijitokeza mara kwa mara kutokea vyama vya upinzani hasa ANC ikiongozwa na Zuberi Mtemvu walihoji uhalali wa madudu yaliokuwa yanafanywa na serikali ya Tanu. Badala ya kujisahihisha Dr.Julius Kambarage Nyerere akaja na mikakati kuuwa kwanza Multiparty ili kuuwa kabisa vyama pinzani, kuuwa Local goverment ,kufidhoofisha vyama vya Ushirika.
Baadae silaha ilikuwa imebakia ilikuwa Elimu,ebu jiulize kwanini wanafunzi wa Mlimani waliandamana hadi Ikulu wakisema AFADHALI YA MKOLONI?unadhani walikuwa hawajui wanadai nini?
Ili kumaliza kabisa upinzani wa wasomi ilikuwa mpango kamambe ambao hadi leo unatugharimu.
Kuvunja nguvu ya communication skills mashuleni akaondoa English
Shule za taasisi za dini zikatwaliwa na serikali.
Syllabus za masomo zikajaa siasa za mwalimu
UPE
Musoma Resolution
N,k
Mkuu mimi siko pale kutengua mawazo yako,ila mimi kwa mawazo yangu naona tunazunguka zunguka,tunajua nani alihujumu maendeleo ya nchi kwa kutetea maslahi yake binafsi ya kuwa kiongozi bila kupingwa kwa miaka mingi.