Mungu anawaona

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
-Kuna wale wasafi wanaojifanya wao ndio watakatifu sana hawajawahi kuchepuka wakati ndio wazinzi mwanzo mwisho Mungu anawaona

-wale wanaojifanya watetezi wa wanyonge wakati mioyo yao imejaa dhambi kubwa ya kuwakandamiza maskini Mungu anawaona

-wale wanaojifanya wapenda haki na wakati kinyume chake ni wenye kuleta dhuruma na migogoro katika jamii Mungu anawaona ,

-Kuna wale wanaojifanya wafia dini na wakukemea maovu ya wenzao wakati matendo na tabia zao ni zaidi ya matendo ya shetani Mungu anawaona,

-wale wote wanaojifanyizia umaskini wa nje na ndani yake wana utajiri wa kutupa kwa mali ya dhuruma Mungu anawaona,


------

Malizieni na wale wote wanaodhani sisi hatuwaoni lakini Mungu anawaona kwa matendo yao.
 
Naona sikuhizi umebadilika MKUU Mungu akusaidie sana na utubu.
 
hahahaha huo ni mtizamo wa kidunia.
mungu hajalishi unamuandika kwa herufi gani anachojali unampa nafasi gani moyoni.
God is a spiritual being and not material being.
Bora umempa jibu mkuu
 
Naona sikuhizi umebadilika MKUU Mungu akusaidie sana na utubu.
Sawa mkuu lakini yesu alisema usinililie mimi bali jililieni nyie na nafsi zenu maana hakuna anaejua kesho.

We unajuaje kama mimi nimeshatubu au bado?
 
Kwa ujumla unaongelea wanafiki na unafiki wao. Na si wanafiki tu, bali yeyote anayemkosea binadamu mwenzie tena kwa kudhamiria, ajue naye yatamkuta.
 
Sitaweka comment yangu kwenye huu uzi

Ila Mungu anawaona wale wote wenye I'D za kile ilihali ni madume.
Bila kumsahau dada mmoja hapa jf niliemtumia nauli na hakuja,,,, mwambieni kuwa Mungu anamuona hata kama anaingia jf kimyakimya [emoji53]
 
Sawa mkuu lakini yesu alisema usinililie mimi bali jililieni nyie na nafsi zenu maana hakuna anaejua kesho.

We unajuaje kama mimi nimeshatubu au bado?
Sina hakika hiyo ni siri yako. Isipokua umekua mwema sasa hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…