Habari,
Mtoto wangu ana miaka 2.3 anaenda 2.4 haongei, nashindwa elewa hii ni hali ya kawaida au kuna tatizo. Alipokua mchanga tuliona ulimi kile kidude cha chini nadhan wanaita udata kama kikubwa tukashauriwa tumpeleke hosp wakakate.
Tumeenda Rabininsia specialist akamcheki akasema hiki hakina shida muacheni tuu ataongea but napata wasiwasi how comes haongei.
Anatamka maneno yasioeleweka, ila maneno yale ni yasioinua ulimi. bababababa, papapapapaa, rarararaaaa hayo ndo maneno yake, neno pekee analoweza ongea ni mma. (maji).
Naomba ushauri, nimsikilizie au nichukue hatua?