Salaam Wakuu, Mbunge wa Mbezi Beach nimekuja tena mbele yenu na kero ya wananchi wangu🌚🌚
Kama mnavyoona kwenye video hapo hapo kuna gari imekwama imekwama asubuhi hii, hayo maji yametuama hapo sababu ya mtaro mbele ya shule ya shule hapo kuziba, kutokana na njia hiyo kuendelea kutumika magafi yamezindi kupachimba na hivyo kutengeneza mashimo makubwa kama handaki.
Sasa kwa jinsi hali ilivyokia magari hayo madogo, watembea kwa miguu, boda na bajaji ni mtihani kupita. Au mnataka kujenga handaki na hamtuambii?
Hiko kipande chote kuanzia hapo kwenye shule kupanda huko juu, hapatamaniki. Huko mtaani ndio utasikia kutapika, yaani mpaka kutoka nje kwenda kwenye kazi zako unapata uvivu jinsi barabara zilivyoharibika.
Na tuliwaambia mapema kabisa wakati wa kiangazi anzeni mapema kurekebisha njia/barabara na kuhakikisha mitaro ipo vizuri kabla ya kipindi cha mvua lakini mlishupaza shingo. Sasa hivi ndio mnajifanya mko bize kuomba barabara bungeni! Zinatusaidia nini wakati tayari tupo kwenye kadhia?
Bunge lililopita baada ya mvua kuharibu njia mliomba pesa, na zikatolewa, sasa nini kilitokea? Gwajima alisema Kawe barabafa itakuwa safi lakini mpaka bunge la sasa hali imezidi kuwa mbovu!
Tunafanywa misukule na bado tumetulia! Embu Wakenya waendelee kutuchangamsha labda tutaamka.