Msaada wenu wakuu

MK 14

Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
25
Reaction score
12
Kuna mdogo wangu alijiunga chuo cha upolisi CCP moshi mwezi wa 8 mwaka 2010 lakini hakuweza kumaliza mafunzo kwani alikuwa terminated mwezi wa 9 mwaka 2010 kutoendelea na mafunzo kwa kosa la kukutwa na simu, baadae miaka miwili yaani 2012 alijiunga na kozi ya Afya kwa ngazi ya diploma na kuitimu 2015, serikali ikatangaza ajira mwaka huu mwezi wa tank akaomba na akapata nakupangiwa kituo cha kazi sasa baada ya kuripoti kituo cha kazi baadae baada ya kujaza detail zake muhimu kwa afisa muajiri akaja akaambiwa eti inaonekana kama alishawahi kuajiriwa serikalini ndipo alipofuatilia wizara ya utumishi ukakuta Tayari alishatengenezewa check number kipindi yuko CCP ! Na check namba iyo inaonesha aliingia kwenye mpango wa malipo yaani mshaara 8/9/2010 na alikuja kuwa terminated 23/11/2010, anajaribu kufuatilia hili apate haki yake lakini mpaka sasa bado hakijaeleweka. Sasa kuna swali la msingi anajiuliza iweje awe na check number wakati alifukuzwa chuo? Ndugu wakuu humu jf nakujaa kuna watu wazuri na waliobobea katika kutoa ushauli angalau ya kimawazo naombe msaada kwa hilo ?
Natanguliza shukrani, naomba kuwasilisha
 
Huyu alikuwa kati ya wale waliokuwa wanalipwa ila hayuko kazini Wafanyakazi hewa, mimi nahisi afuatilie wizarani akawaambie ukweli ilivokuwa
 
Inasikitishaa sana; hafukuzwe mafunzo yeye alafu Leo inaonekana alikuwa na check namba na pesa ikawa inaflow wakati ajawahi lamba ata senti moja ; kwann watu wanawasababishia matatizo wengine ambaye hakujua lolote lile
Huyu alikuwa kati ya wale waliokuwa wanalipwa ila hayuko kazini Wafanyakazi hewa, mimi nahisi afuatilie wizarani akawaambie ukweli ilivokuwa
 
Kuna mtu anatumia jina lake kula mshahara, mwambie dogo afatilie hadi wizarani haki yake itapatika tu.
Kesi ndogo sana hii.
 
Mkuu kashafatilia mpaka pale utumishi response yao wanasema wanalishughulikia mpaka sasa miezi mitano imepita anasubiria majibu
Kuna mtu anatumia jina lake kula mshahara, mwambie dogo afatilie hadi wizarani haki yake itapatika tu.
Kesi ndogo sana hii.
 
Mkuu kashafatilia mpaka pale utumishi response yao wanasema wanalishughulikia mpaka sasa miezi mitano imepita anasubiria majibu
dah yawezekana hapo utumishi ndo walewale, fanyeni maamuzi magumu ikiwezekana fika mahakamani au tafuta contact ya waziri husika.
Hapo utumishi anaweza akazungushwa mpaka Magufuli anatoka madarakani.
 
Kuna ndugu yangu kaambiwa hawezi ajiriwa sababu hana cheti cha Mwaka mmoja wa Nursing akati ana cha miaka miwili... Ila nahisu kabisa kuna mchezo anachezewa hapaaa... Tanzania hapana jamani rushwa na roho mbaya haziji kuishaa...
 
An
 
Yaah zinaruhusu mkuu...!! Yani aliomba kazi akafanyiwa na interview kabisa akajaza na mkatabaa.. mwishoni HR sijui anamwambia hawezi pata cheque namba kisa hana cheti cha mwaka mmoja... akati toka mwanzo kapita vizuri hadi mwisho kabisa ndo anapewa hiyo sababu...! Hapa naona kuna mchezo kachezewa maana ingekuwa hawaruhusu angeambiwa mapema...
 
Alisoma chuo gan?
Private? Government?
Na hyo gap,,,wanapo zungusha n private or?
alisoma government mkuu...! hapo anapozinguliwa ni government kaka.. ajira mpya hizi
hapa anawaza kuandika barua ofisi za Utumishi...
 
Okay!!!
Kama alikuwa na vigezo vya kusom hyo koz & Kama alipat credit poa kwahyo certificate nivyema2 afanye hvoo!!!!
Labda Kam aliingi@ kiujanja ujanja broo Mambo yatakuwa magumu upandewake!!!!!
But inatakiwa afanye Mambo kwa uharisia na uhakika Kama yalivyo
 
Sawa mkuu
dah yawezekana hapo utumishi ndo walewale, fanyeni maamuzi magumu ikiwezekana fika mahakamani au tafuta contact ya waziri husika.
Hapo utumishi anaweza akazungushwa mpaka Magufuli anatoka madarakani.
 
Nadhani ndo hivyo bro..ila alisoma kabisa hiyo certificat ya miaka miwili nursing..!! Saaa hii wanataka mwaka mmoja ndo duuh msala huu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…