baraka muyabi
Senior Member
- Aug 13, 2012
- 162
- 58
Ndio maana nimeshindwa mkuu mpaka kuomba msaada ...yamenifika shingoniduh kumwaga oil kila baada ya wiki???[emoji15] [emoji15]
Shukrani mkuu ngoja nijipange maana nimeumizwa mpaka akili imenikaa sawaBaraka, mafundi wengi hawana uchungu na mali ya mteja. Wao wanachojali ni kuingiza siku. Wengi wanataka urudi kesho na kesho kutwa.
Nadhani baada ya kuchemka, alienda kuomba msaada kwa mafundi wengine, ndiyo maana akakwambia ubadili engine. Off which yupo right kabisa.
Ukitaka hiyo issue iishe kabisa, nunua engine ya 3S, nadhani kwa sasa itakuwa kwenye 1.6m ambayo ni complete pamoja na vikorokoro vyake. Au unaweza kununua "mswaki", ambayo ni engine tu bila makorokoro yake kama vipipe na kadhalika. Nashauri ununue complete.
Ikiwezekana nunua kwenye maduka wanayoagiza kutoka nje ya nchi kama beforward. Usije ukauziwa engine ambayo imefanyiwa overhaul.
All the best mkuu.
Nashukuru kwa ushauri ila nipo Mwanza mkuu...Kama upo dar njoo gerejini kwangu ukonga banana nikutatulie tatizo lako nimeshakutana nakesi hizo marakibao nakila niliemtengenezea hakurudi natatizo hilo tena
Hio engine ni D4 or D4 vvti? Kama una uezo kununua engine ya 3S ndio solution ya uhakika Kibongo bongo, pia ukipata d4 at a good price take it, mana d4 inahitaji matunzo, ukiijulia hata Mafuta inatumia Kidogo Kiliko 3S...tatizo lako ni dogo na linatengenezeka ukipata Fundi Mzuri na ukawa mvumilivu (Mm hua yananishinda mana mafundi wengi wababaishaji, una change Spares Moja bada ya nyingine mpaka Tatizo lipatikane)Habari wana jamvi wenzangu...nilikua naomva msaada wa kiufundi katika engine ya gari aina ya Nadia. Inachanganya sana oil na petrol yaani naweka lita 3 za engine oil ila baada ya wiki moja namwaga lita 6 mpaka 7 (maelekezo ya fundi nimwage kila baada ya wiki)...fundi kasema tatizo ni pump..nimebadili pump nikaweka mpya bado tatizo ni lile lile. Inawaka kwa siku moja siku ya pili haiwaki..inatoa moshi mweusi ajili ya kuchanganya oil na mafuta.sasa fundi kaniambia nibadili kabisa engine niweke 3-S , kiukweli simuamini tena fundi maana nimeumia vya kutosha na tatizo haliishi..msaada tafadhali je ni kweli kubadili engine ndio suluhisho au..Nawasilisha
Kirumba mkuuUmetengenezea maeneo gani?nikushauri fundi mzuri. Kama ni mafundi wa pale Sahara umechemka
Shukrani mkuu LEGE ngoja nilifanyie kazi ombi lako maana huu usawa kupata milioni unatambika usiku mchana ..na bado usawa hausomiMnao mshauri kuwa aachane na hiyo engine na nyie ni mabashite tuu na vichwa maji.
Mkuu pole sana sana sana sana.kwa upande wangu mm nakuonea sana huruma aisee.hiyo unayotaka kufanya haikubaliki huwezi ingia garama ya zaidi ya milioni kwa usawa huu wa magufuri tena garama hiyo na kuliharibu gari lako maana alicho kushauri na wanachokushauri wadau hapa cha kuweka engine ya 3s ni uharibifu wa gari kabisaa.na utaingia garama mara 2 ya kununua engine nyingine ya d4.
Kurekebisba huo ugonjwa garama yake haizidi hata laki 2.
Kwenye gari yenye engine ya d4 sehem ambayo kwa asilimia 99 huwa inafanya mafuta kuingia kwenye engine na kuchanganyikana na oil ni kwenye d4 pump .
Jaribu kupeleka gari gereji nyingine au tafuta fundi mwingine pia.ili aweze kutatua hilo tatizo lako ni tatizo dogo sana lkn ukisikiliza ushauri wa kununua engine nyingine itakuumiza ww na kama unanunua basi kanunue hata half engine a.k.a mswaki tuu.kama hiyo itakuwa ishaharibiwa na mafuta
Mkuu, tulizana akili ndiyo uchukue maamuzi. LEGE ametuita mabashite, lakini mimi nimezungumzia experience.Shukrani mkuu LEGE ngoja nilifanyie kazi ombi lako maana huu usawa kupata milioni unatambika usiku mchana ..na bado usawa hausomi