Habari za humu na heri ya Mwaka mpya 2021.Mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 25 mkaazi wa hapa jijini dar es salaam.Nina elimu ya shahada ya kwanza ya uhandisi katika chuo kimoja wapo hapa Dar.Naamini humu JamiiForums kuna wataalam au watu ambao wanaweza kunisaidia au kunipa ushauri ambao utanisaidia katika hali yangu ya afya ya akili.Hizi ni baadhi ya dalili.
Mimi ni mtu wa kuwa ninapenda sana kukaa peke yangu,yaani i feel much comfortable ninapokuwa peke yangu,lakini cha ajabu unakuta baada ya kuwa peke yangu I just feel lonely tena deep lonely.
Pia nimekuwa mtu wakuwa nakosea sana katika maamuzi mengi ninayofanya,yaani kukiwa na jambo ambalo natakiwa kuamua nakuta naamua then matokeo yake yanakuwa mabaya kana kwamba yamefanywa na mtu asiye na akili vizur,hii inafanya sana kudandia au kuamini sana watu katika kufanya maamuz kwa sababu nahisi nikifata ubongo wangu ntatoa results mbovu.
Tatu ni mtu mwoga sana na kushtuka kwa kitu kidogo tu,yaani kitu kidogo naweza nikapanick hata bila sababu kubwa halafu nikicalm naanza kujishangaa kwamba mbona hakukuwa na reason ya msingi ya kupanick vile.
Nne,ni mtu ambaye nakua bored au naona kero kwa mtu ambaye anaonesha upendo kwangu au kama mtu akiwa ananijali naona kama ananisumbua hivi,kimsingi mtu akiwa anakupenda ni kitu kizuri na cha kujivunia ila kwangu hua naona tabu na kero.
Nilishawahi kwenda hospitali kwa watu psychology katika hospital moja hapa dar sikupewa ushauri Bali nilipewa Dawa aina ya resperidone ambazo nilikunywa siku moja tu na nikaziacha kutokana nahisi zilitaka kuniua sikulala siku hiyo na nikaacha kabisa kwenda hospital.
Hizo ni baadhi ya dalili japo sio mwandishi mzuri naamini wasomaji au wachangiaji mtaelewa au kama hujaelewa I can clarify ili mradi niweze kupata msaada kijana wenu.