Habari wakuu,
Nilinunua king'amuzi cha Azam wiki iliyopita,TV yangu haina option ya audio out,sasa nikaunganisha waya wa audio kutoka kwenye king'amuzi kwenda kwenye subwoofer,cha kushangaza king'amuzi kimekaa siku sita tu afu kikagoma kuwaka..afu kilikua kinapata moto sana kuliko kawaida.
Kuna mtu ameniambia et subwoofer zinatabia za kurudia umeme kwenye sehemu ya sauti inakotoka ndo maana huunguza deki na vitu vingine.Naomba msaada wenu ni kipi naweza kufanya ili kuzuia tatizo hili?
Natanguliza shukrani zangu
warudishie AZAM TV kama ni s/w issue watafanya kui flash na Stock rom binary file au kama ni hardware issue wata fanya repair au wakupe kingamuzi kingine
Nilishakorudisha kaka,na wamenipa kingine....Lakini sasa natafuta suluhisho la hili tatizo.Km kuna kitu niachoweza kutumia ili king'amuzi kisiharibike tena
Nafikiri hapo ushauri huyo jamaa juu ndo utakufaa maana wengi wamelalamikia subwoofer kuharibu vifaa vyao zikiwemo hadi simu kuishiwa betri haraka na kujizima zima
Fanya utaratibu ufanye connection ya kingamuzi na TV directly
Home theatre ni shillingi ngapi mkuu?
Cheapest home theatre za Sony ni 220,000/-. Ni nzuri though. Ukiwa na Home Theatre hayo matatizo ya kuungua DVD players au ving'amuzi utayasikia kwa jirani.
TV yangu haina audio output....so kwa hiyo Home theatre hazina madhara kwa king'amuzi...maana nitaunganisha king'amuzi na home theatre
Hiyo TV haina HDMA? coz ungenunua cable yake na picture quality ingekuwa poa hadi ungeshangaa, ungeunganisha decoder na tv set kwa HDMA cable, then cable moja (ya picha) toka kwa DVD kwenda kwa TV ili ukiangalia movie isiwe shida. Simple!!