Msaada: Nasumbuliwa na vipele kichwani

CHITAKO

Member
Joined
Jul 13, 2017
Posts
31
Reaction score
10
Nasumbuliwa na vipele kichwani,vinawasha na kuuma pia vinatoa usaha kwa mbali,nimepima gonjwa letu nipo salama vinatokea hasa baada ya kunyoa na nywele kuanza kuota ni muda mrefu takribani miaka 3 sasa naombeni msaada kwa anayejua dawa,ama ushauri.
 
Aisee hata mi mimi nina changamoto hiyo,ngoja waje wajuvi
 
Wewe bado ni mtoto? huwa naona watoto ndio wanapatwa na hilo tatizo
 
Naona wataalamu hawakupitia hapa. Mi mwenyewe nasumbuliwa na hili tatizo,nimeshapiga dozi za kutosha lakini siponi.
 
Nadhani watabibu wa hapa Tanzania hawana majibu ya hili tatizo.
Hili tatizo huwapata watu wazima na utakuta wanatumia dawa nyingi bila kupona.
Tuendelee kusema hadi hapo watakapopatikana wenye kuleta ufumbuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…