Wakuu habari...
Modem yangu kwa siku ya pili mfululizo haisomi katika kompyuta yang na hivyo siwezi kuunga ili kupata internet, nilijaribu kuiunistall mwanzo na kuinstall upya haikufua dafu, baadaye nilifanya system restore lakini wapi, na hiv sasa nikijaribu kuiunstall inagoma kabisa kutoka, nimetumia cc cleaner kuiondoa pia imegoma kutoka na inaniletea ujumbe huu: is not a valid integer value, access violation at adress 000003DC,
Tafadhali msaada wako ama mbinu nyingine unahitajika kuokoa jahazi
Natanguliza shukrani
mara ya kwanza ilipogoma kusoma ilikuletea meseji gani?
mwanzo kabisa ilikuwa inafunguka lakini ile sehemu ya kuconnectambyo huwa na rangi nyekundu nikiibofya inagoma ku-connect na hivyo nikafika uamuzi wa ku-uninstall na kuinstall upya. Baada ya hapo sasa ndo nakutakutana na ujumbe huo juu.
Ahsante
window 7 mkuu
Dial up imezingua mkuu...
fanya ivi tafuta modem nyingine ujaribu kuconnect ikigoma uninstall hiyo software alafu install upya kwa kutumia ile modem nyingine ikigoma pia ujue kuna tatizo kwenye port unachotakiwa kufanya tafuta dc unlocker alafu tafuta sehemu iliyoandikwa enable ports utaona modem yako inaji restart ikigoma pia kuconnect jaribu kwenye pc nyingine pia ikigoma ujue modem itakuwa imearibika
Mkuu nafikiri drivers za internet connection ndizo zinazoleta shida kwa sababu leo nimejaribu ku-connect kwa ttcl broadband imegoma mazima, vile vitaa vinavyowaka mara baada ya kuinstall cable yamodem ya ttcl havikuwaka na kila nikifanya dial up sikufanikiwa. Pia modem hii nikiitumia kwa conputer zingine ina-perform vizur bila shida