Mkuu kuna vitu vinne ambavyo huyu mtu anatakiwa ajue.
1. Anataka kufungua dispensary, health center, specialized clinic au hospitali? Kwa jinsi ulivyosema nadhani atahitaji kufungua dispensary. Ila naamini staff uliowataja ni wachache, la sivyo afungue maabara tu.
2. Anataka kufungua wapi? Nijuavyo ni kwamba kituo cha tiba kipya kinatakiwa kiwe na umbali usio chini ya km 5 toka kilipo kituo kingine cha tiba.
3. Kabla hajajenga au kufanya ukarabati, lazima aende kwanza kwenye ofisi za daktari wa wilaya au manispaa au jiji ili waweze kukagua eneo na kukupa ruhusa ya kuendelea na mipango ya ukarabati. Hii ni muhimu sana, maana ni kawaida kwa watu kukataliwa eneo walilojenga au kuambiwa wafanye marekebisho makubwa kwa sababu tu hawakuchukua ushauri kabla ya kuanza ukarabati.
Hapa pia kuna umuhimu wa kufikiria disposal ya taka. Vituo vingi vya tiba huingia mikataba na hospitali kubwa katika kuteketeza taka. Hili ni jambo la muhimu sana. Na huyo mtu lazima identify mahala atakokuwa ana dispose taka zake au kama atajenga 'insinereta'.
4. Kila kituo cha tiba sawasawa na mnyumbulisho huo hapo juu namba 1, huwa na mahitaji ya chini ya aina ya wafanyakazi, majengo na vifaa. Hivyo ni vyema uende ofisi zilizotajwa hapo namba 3 ili uweze kuelezwa mahitaji ya chini ya rasilimali watu, vifaa na majengo na hata taratibu za usajili ambazo pia huanza hapohapo namba 3.
N.B
Ukishamaliza ukarabati, kuna fomu nne wazijaza na kuzitengeneza kama kitabu, ambazo zitapelekwa wilayani, mkoani, na wizara ya afya hatua kwa hatua. Copy moja itarudi kwako.