Jana niliwahimiza sana Chadema kwenda Ulanga magh na Kilombero, msingi wa hoja yangu ilikuwa hili ombi la thread. Kule Ulanga Magharibi pongezi ziwaendee wanafunzi wa SUA walioamua kwenda kumsaidia prof Mlambiti, niliwaandikia chadema kuwa wanapaswa wakamsaidie mzee Mlambiti kwani naturally si mtu wa majukwaa, watu wale walikuwa tayari kwa mageuzi kilichotakiwa ni booster ya kuweka uhai wa hoja za prof Mlambiti, SUA students waliweka kambi Malinyi na kwakweli walifanikiwa sana, kosa walilolfanya walipoamaliza kampeni wengi wakabaki malinyi kumbe walipaswa kuweka kambi mtimbira kudhibiti uchakachuaji kwani pale ndio centre ya vitendo hivyo.