Mnyika ataka vijana kujiajiri

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewataka vijana kutumia fursa ya kujiajiri katika ujasiriamali, ili kuondokana na umaskini.
Mnyika alitooa ushauri huo jana wakati akitoa zawadi kwa washindi wa mchanganuo wa biashara kwa vijana wasio na ajira na waishio katika mazingira magumu yaliyoratibiwa na asasi ya maendeleo Ubungo (UDI).
Alisema wakati umefika kwa vijana kutumia fursa ya ujasiriamali katika kuendesha biashara mbalimbali.
Alisema vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo sekta ya ajira, hali ambayo inahitaji vijana kutumia maarifa binafsi ya kufanya ujasiriamali katika kuondokana na umaskini.
Alisema washindi walioandika mchanganuo kutumia vizuri ubunifu katika kujikita katika biashara katika kukabiliana na umaskini.
Kwa upande wake, Ofisa Uwezeshaji wa UDI, Goodluck Justine, alisema shindano la kuandika michanganuo limedhaminiwa na Mnyika ambalo ni la thamani ya sh milioni moja.





source: Tanzaniadaima

[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Chalila Kibuda


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
 
Tatizo kubwa ni mitaji na elimu ya kuona opportunities mpya........ila vijana tuna hali ngumu sana aisee........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…