Mnaionaje hiyo nyumba?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
Nyumba inauzwa ipo maeneo ya Tandika Azimio. Ina vyumba vitatu vya kulala, bafu, choo, jiko, sebule. Ipo barabarani kabisa na hivyo kufaa kwa uwekezaji wa fremu za biashara za kupangisha au kuweka bar. Ina umeme na pia ina hati. Bei ni Tsh. milioni 35. Kwa wanunuzi wenye hitaji, piga simu

​



​

​

​
<center>TOA MAONI YAKO HAPA CHINI</center>
 
Na huenda mtu anaingizwa mjini maana iko barabarani sana! Hukawii kufa kwa presha baada ya kuinunua halafu asubuhi una kuta tinga tinga limesimama nje.

Nafikiri hiyo barabara ni mojawapo ya zile zinazotarajiwa kupanuliwa
 
Mbona kama iko chini ya High Tension Line ya Tanesco, ilipataje umeme?.

Hapana sio HT ni umeme wa kawaida, ila ukiihitaji inabidi uende ardhi ukajiridhishe kwanza hasa kwa ramani mpya za mipango miji, watu waliumizwa sana kwenye upanuzi na ujenzi wa njia ya ubungo maziwa
 
Na huenda mtu anaingizwa mjini maana iko barabarani sana! Hukawii kufa kwa presha baada ya kuinunua halafu asubuhi una kuta tinga tinga limesimama nje.

Hivi unaweza kununua ardhi bila ya kuwa na ramani ya block husika kiongozi??!!!!
 
Kwa mi ni shida huko uswahilini ni kutwa na kuchwa ni vibaka tuu na hasa ukifunga dishi la azam ni kosa kama vile ulewaita mi labda msasani ndo poa na sijali bei
 
Hivi unaweza kununua ardhi bila ya kuwa na ramani ya block husika kiongozi??!!!!

Mkuu.

Kwa mipango ya serikali hii lolote linaweza kutokea mkuu, kwani hao wote wanao bomolewa kila kukicha ulidhani hawana ramani ya block husika? Au umesahau kuwa kuna wanao tekeleza mipango waliopanga na wake zao
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…