Mke wangu simuelewi!

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
2,766
Reaction score
1,716
JF ndio kila kitu kwa ushauri,mafunzo nk
Kama mnavyojua maisha ya ndoa yana changamoto zake,hayafananishwi na mstari ulionyooka bali ni kona kona nk.Hivi karibuni mke wangu amekuwa akinitolea maneno nisiyoyaelewa,ikitokea kutofautiana kati yangu na yeye anadai anafanya kitu ambacho sitakisahau.
Jana jioni alirudia kauli hiyo baada ya kutofautiana kuhusu mipango ya maisha hapa nyumbani kitu ambacho kwangu ni jambo la kawaida. Nilimuuliza hicho kitu unachotaka kufanya ni vipi?au unataka kunnitoa roho?hakutaka kunijibu lolote kiasi kwamba naanza kuwa na wasiwasi wa kulala naye chumba kimoja.
Nawaombeni ushauri wana MMU,nichukue uamuzi gani?kwa maana hata kama uamuzi wake ukawa kujua yeye bila shaka sitakuwa salama!
 
Keti chini,msikilize zaidi ya kuongea,kile anachokisema kama ni cha kujenga kifanyeni,kama hakifai mweleze mpe na sababu za kushindwa kukifanya,
wanaume wengi mnaona matatizo kwa wake zenu huku tatizo limeanzia kwako,..
 
Keti chini,msikilize zaidi ya kuongea,kile anachokisema kama ni cha kujenga kifanyeni,kama hakifai mweleze mpe na sababu za kushindwa kukifanya,
wanaume wengi mnaona matatizo kwa wake zenu huku tatizo limeanzia kwako,..

Missc u
 
Maneno ya jazba tu hayo, Jazba zikiisha na yeye anasahau yote aliyoyasema
 
muanze kwenda wote katika nyumba za ibada pamoja
 
!
!
acha uoga mtu wangu la sivyo utachanganyikiwa. Akifudia tu kauli hiyo mwambie maneno haya tena kwa kumaanishu, "mke wangu, tumefanya mengi sana ya kukumbukwa. Hilo unalotaka kufanya halitaleta tofauti kubwa sana na isitoshe mimi ni mtu mzima na nimepitia mengi. Fanya lipendezalo nafsi yako" .....
iriplesabo ni fikura tu.....dont chase just replace or ride it solo.
 
Ndoa bwana.

Kama kipato cha mumeo hakikuridhishi si uondoke zako?

Kumpa presha mtoto wa watu kwa vitisho kisa nini?

SMDH!
 
kumbuka huyo ni mke
ongea nae kwa upendo ili kukata sumu ktk mahusiano yako anza kufikiria utatuzi wa chanzo cha matatizo yote!
 
Hebu tuliza ball fikiria ulikosea nn. Nini kinaweza kuwa chanzo mpaka mmefika hapo. utapata majibu tu I believe. Mchukue kama una uwezo nenda nawe beach kali. Ukibifi mlale out of the common ground. Mpe mapenzi na feelings zote. Wala usigusie ugomvi katikati ya safari atafunguka tu.
 
Kabla sijakushauri lolote naomba nijibu Je,kabla hujamuoa hakuwahi kuonesha dalili ya tabia unayoilalamikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…