Mabaya na mazuri, ndiyo sifa ya ubinadamu/
Na kuzama kwenye kaburi, ndio mwisho wa hatamu/
Alikuwa mashuhuri, na hata umtukane anatabasamu/
Ila ukimletea sana jeuri, fact utazikuta Instagram/
The Kokobanga, visu juu ya gadem visu/
Dah! Mungu amepanga, machozi kwenye tishu/
Ulituhusia tupige kazi, 5 star hayo mambo ni gharama/
Ukatupa hasira za wazi, ili tukazane kupambana/
Hukupenda uduanzi, anaekosea ulimchana/
Hata aogopewe na shazi, hukuhofia mlivaana/
Pumzika Gademitti, Mungu akupokee vyedi/
Waliokuandama na mtiti, ulishawaambia case closed/
Kaburi halina mazoea, ameshalala tunapaswa kumuombea/
Alikua mshkaji, rafiki lakini mbabaishaji/
Anakula leo anasahau kesho, alijiona sana spesho/
Gademu five star, downtown mjanja ndani ya dar/
Story nyingi za degree tatu, mabaharia sio watu/
muongo yani beautiful liar, hakuna aliyemu-inspire/
Hakuona mbele kutwa misele, pesa kidogo nyingi kelele/
nachana tena kiunderground, nimeshika sana dollar na pound/
akili kubwaz bebez, hakai mbali na swekeni meen/
mfalme wa insta kapigana kila vita, jf, fb na twitta/
yameshapita namuombea, kile neno tushaongea/
tumuache mbele ya haki, mimi na wewe hatujui nani atabaki/
kifo ni lazima iwe. leo kesho tunapaswa kujipima/
bata kidogo, shika sana neno la uzima/
ardhi inameza haitosheki, zamu kwa zamu usijione keki/
stay positive be humble, never lose focus life is a jungle/
wazuri wabaya roho ni mlango, moyo kichaka na pango/