Killing machine
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 2,396
- 3,436
Siku hizi ukiona bila woga, demu kapost eti aolewe/Niite Mzee Mpili, maana Jamii Forums nina watu/
Ukinikosa jukwaa hili, nipo uzi wa warembo wanaoshika safu/
Chit chat kwangu sio dili, maana wana mambo machafu/
Habari mchanganyiko siwezi subiri, japo kila muda habari za wafu/
Mauaji yamekithiri, mara moto mara risasi za mapafu/
Kule MAHUSIANO sio shwari, kutwa kuwaponda madem halafu/
Ndio hao hao wanaanzisha habari, Pm kwa watoto wa watu/
Kule SIASA ni mabishano makali, usiwaamini hata washike Msahafu/
Na nimeshaizoea hii hali, JF kila mtu ana Sarafu/
Mistari bampa to bampa, niliishia kwenye ngumu nyeusi/Rhymes zangu Al Shababi, napiga kwenye shingo/
Watoto beki hazikabi, wamekimbia ulingo/
Manyota 'inchaji', mi' suka mi' utingo/
Wako wapi wafa maji, niwamalizie na tindo/
Hawataweza kupima, mi nacheza na vina/
Natembeza mboko/
Nawapoteza mazima, wanageza kama China/
Na wanatoa boko/
Mvumbo ni zawadi, kwenye hiki kizazi/
Cha watoto wenye midadi, halafu wali nazi/
Wanakuja wanajinadi, tena shazi/
Ila ninapotema radi, wananiita mkuu wa kazi/
Game dakika tisini, ila life jihadi uelewe/
Maana hata mke wa masikini, kuwadi mumewe/
View attachment 1619670
Asante mvumbo we Ni mkali wa hizi kazi/Mistari bampa to bampa, niliishia kwenye ngumu nyeusi/
Tayari Mvumbo nipo hapa, nachana zaidi ya Msusi/
Hii ni bahari ya mapapa, dagaa hakikisha haugusi/
Na ukileta shanapa, usije ukatuona ni nuksi/
Hatufanyii hii kwa kutumwa/ kusukumwa/
Wala utumwa/ ila tusipo Rap tunaumwa/
Hivyo vina siyo vya kuchanga, ni kisanga ni faya/
Mistari naipanga, zaidi ya shanga kwa Malaya/
RIP Zilla na Albert Mangwea/Asante mvumbo we Ni mkali wa hizi kazi/
Kitambo tu nakusoma we Ni noma iko wazi/
Leo nakupa tano ile ki nunda Kama Daz/
Oi oi ka saigoni sema hawakusomi vichwa panzi/
Naandika nasikitika jinsi zilla alivoacha pengo/
La freestyle Ila sikuhizi naona yupo kado kitengo/
Acha niishie hapa nimeshea tu mapendo/
Tukutane tena mwakani kwa Leo nimemaliza mwendo....
Enzi za michano/ tenzi volcano/ sipotezi mapambano/Weita leta vikali, nitulie niache nishai/
Maana ndonga imejaa mistari, zaidi ya shuka ya Kimasai/
Ndio maana sina habari, watoto wanapojidai/
Wananipandisha morali, nipo ni vipi wanajimwambafai!?/
Hii ndonga/ ninapobonga/ kwao ni skonga/ acha wasome/
Game kwangu kitonga/ nasonga/ wanachonga/ na washafika ngome/
Ona macho pima, nilipo hawawezi timba/
Nacheza na vina, ka' Masai na Simba/
Dogo kaja juzi tu leo analeta dharau/Heshima yangu naikamata, maana kelele nyingi/
Wanam diss Dizasta, kisha wanajiita King/
Madogo ni wa kuchapa, hawastahili hii ring/
Tayari Mvumbo nipo hapa, mimi ndiyo mtunza misingi/
Ya huu utamaduni/ dhidi ya Crew za kihuni/
Wanaowekwa juu na Mawinguni/ nikisema suu waje miguuni/
Wanaharibu Culture/ anajaribu Rapcha/ ila hayupo karibu na Dizasta/ hivyo taratibu anapaswa kufyata/
Kusifiwa kuchana, leo madogo wana pretend/
Mkubwa unamtukana, na bado anakuita Best Friend/
Dogo gani unayemsema yule anayependa visa/Dogo kaja juzi tu leo analeta dharau/
Analeta utata atazikwa tutamsahau/
Dizasta ana Vina vya kuuwa career ya Cosmas/
Tribulation alimcha kuwa hajui hata BODMAS/
Kuijua Bange et leo anainyea kambi/
Bora afanye udaku aungane na Mange Kimambi/
Nna mengi ya kusema subir nikijipanga/
Kwa sasa niko kweny basi naelekea Shinyanga/