Little brain
JF-Expert Member
- Oct 31, 2020
- 4,395
- 6,556
Aliesema bongo bahati mbaya apewe kret la safari maana aliona mbali../Hii nchi bado inaujinga mwingi, vitu bei juu afu eti mama anaupiga mwingi.../
Viongozi wengi bado ni walowezi, kutoka ngazi ya kata hadi wakurugenzi.../
Ni mafisadi kiufupi ni wezi, kodi za wanachi wanazila bure kila ifikapo mwisho wa mwezi.../
Mgao wa umeme naskia umewekewa ratiba, aisee huu uongozi hautufai ebu tupeni katiba.../
Tozo za miamala zimeongezewa riba, uamuzi ni wako kukaa na govi au kumfata ngariba.../
Hatukutafutana, kila mtu kivyake hakuna kujuana.../Alikuwa ni mtu wa church, hapo ndio nikajua kumpata itakuwa kazi.../
Nilikuwa tayari kwa lolote nimpate, miondoko yake na upole vilinifanya nidate.../
Siku moja alikuwa anakatiza sokoni, nikamfata kumueleza namna alivyonikaa moyoni.../
Akashangaa akauliza kwani kulikoni, unanipenda mimi kwani wengine huwaoni?.../
Nikamwambia mama usiwe na hofu, nakupenda wewe wengine siwaoni nimekuwa mpofu.../
Basi nikamjaza maneno kumpa hope, maana nishachoka daily kutumia soap.../
Akanipa namba tukaaza kuchart, kesho kutwa nikamualika club ku party.../
Akasema hiyo ni dhambi mi nimeokoka, lakini dingi pia ni mkali nikisepa atafoka.../
Nikamuambia we ni nguzo ukiacha nita dondoka, sitaki uwende mbali maisha ya upweke nimechoka.../
Lakini haikusaidia maana aliniaga kuwa anaondoka, anaenda mkoa wa mbali kusoma.../
Akaniahidi kunipa ushirikiano every day, lakini alivyosepa simu zangu akawa hapokei.../
Sometimes akipokea ananikalipia, kuwa nimekuwa kero ameshindwa kunivumilia.../
Nimpe muda nipunguze simu kumpigia, atanitafuta kwa muda wake yeye akisikia.../
Aliambia mengi ya kuudhi, aliniambia nitafute demu mwingine sinabudi.../
Masta nikasema huo ni ushenzi, vipo vya kuhangaikia ila sio mapenzi.../
Nikaacha kutuma meseji, hata nikituma nikawa simuiti baby.../
Kuviziana ndio ikawa mbinu, kila mmoja anamsikilizia mwenzake apige simu.../
Sio siri ilikuwa ni zaidi ya mafarakano, ilipita miezi sita bila mawasiliano.../
Fanya kumpotezea, ukomae na msoto/Hatukutafutana, kila mtu kivyake hakuna kujuana.../
Japo kupitia whatsap niliziona status, mara nyingine anipige vijembe mpaka basi.../
Kuna siku moja alipost nikaona dalili, kuwa tayari kashapata bwana wapili.../
Sikutaka kuumiza kichwa, kwani kila siku alikuwa akipost picha.../
Status ziliwekwa maneno ya nyodo, eti chini ya mnazi kaokota dodo.../
Sikuwa na wivu nilimuacha atambe, alisema ana date na wasomi sio waliokimbia umande.../
Mwanzo alianza kumuita class mate, na kuwa wamefaulu na kupata the same grade.../
Hajui mi kwake nishafunga gate, hata anitambie vipi haniumizi head.../
Akapost eti walokole wakidate, hawapaswi kuitana baby.../
Akamtag na jamaa kimafumbo, akampa sifa za mambo lundo.../
Siku zikapita, upepo ukabadilika.../
Status sa huzuni zikaongezeka, kuonesha kwenye hilo penzi anateseka.../
Zile status za kejeli zilikoma, kuonesha hata yeye namba anaisoma.../
Unanipa faraja najiskia furaha mno, navyoona ukitoa ushauri kwa mistari ya uno.../Fanya kumpotezea, ukomae na msoto/
Maisha ni safari haziishi changamoto/
Unapovunjwa Moyo unaujenga tena/
Usiweke chuki acha iondoke na iende Vyema/
Wanasema hakuna mapenzi bila pesa, japo wenye nazo nao wanateswa../Unanipa faraja najiskia furaha mno, navyoona ukitoa ushauri kwa mistari ya uno.../
Kiukweli sina chuki, japo moyoni kaniachia jeraha la mkuki.../
Nasonga mbele ya nyuma sikumbuki, alijidai mlokole kumbe mamluki.../
Kama mapenzi pesa, basi hiyo ni biashara.../Wanasema hakuna mapenzi bila pesa, japo wenye nazo nao wanateswa../
We ni mtu mzima yakupasa kulinda heshima uliyoiweka kabla hujazeeka../
Mapenzi ni hisia anae kuchukia ipo siku atakulialia, ndio maana hata Biblia inatuhasa kuvumilia../
Kuna muda wa kucheka na kulia, ila tambua hakuna jipya chini ya jua na hiyo ndio dunia../
Naanza kukuchana kwa kusema "Mazafaka",Naitwa makovu a.k.a machata, kichwani sina dread afu peace zaid ya marasta.../
Usinipeleke kule hapa ndio napo pataka, pana msosi kibao si unajua leo pasaka.../
Weka amila kiumuke kikando, kwa mkapa tujumuike kumzoea orlando.../
Hii ni mission ya wana appolo, Simba atashinda hata wakinuna utopolo.../
Heshima kwako yuda,kumbe nawe wayajua./Aliesema bongo bahati mbaya apewe kret la safari maana aliona mbali../
Nchi imepwaya kila sekta, maskini hawana hali wanashindia ugali na kachumbali../
Hakuna michongo wala ajira, vijana wanafilisika kwa kamari/
Rais kapagawa taifa lipo chini ya utawala wa uza madawa../
Tumekubali tuna vuna tulichopanda, ila tayari wingu limetanda 2025 tumejipanga kwa mapigano/
Sichagui Mbususu, na wala sina matabaka/MARA 1 KWA MWAKA challenge
Kuna vingi navifanya hata bila utata, nikikosa mboga nakula panya hadi siku ya pasaka.../
Huku ukiona tumejazana ujue kinawaka, hakuna mambo ya kusemana-semana/ maana kukutana ni mara moja kwa mwaka/
Kwetu tunapenda umoja marufuku matabaka, jenga hoja acha vioja kama mtu aliedata/
Jf kuna pisikali ila ni ngumu kuzipata, bila shari natongoza mpaka wife wa askari kisha namchakata/
Marapa wengi hawafai couse verse zao zimechacha, hawana mistari thats why wanapga show mara moja kwa mwaka.../
Mara moja kwa mwaka huwa nashinda jamvini na wana-board, tunajadili kuhusu vibaka wa mjini na ongezeko la panya-road.../Sichagui Mbususu, na wala sina matabaka/
Kama ya mke wa mtu, nachakata mara moja kwa mwaka/
Kwa changudoa sijitusu, maradhi na mashaka/
Na danguro likinihusu, ni mara moja kwa mwaka/
Mc's wanachana nusu nusu, wakigundua nipo hapa/
Kuwakilisha nitawaruhusu, mara moja kwa mwaka/
Nyuki huwezi kum'busu, japo asali unaitaka/
Hivyo Ex kumywea Al kasusu, mara moja kwa mwaka