Idd Ninga JF-Expert Member Joined Nov 18, 2012 Posts 5,539 Reaction score 4,854 Nov 13, 2018 #1 1.Tulimponda fulani,kwamba anacheka cheka Kila siku yu angani,na madege anaruka. 2.Leo katua jamani,yule alofikirika Ukiuleta utani,ni fimbo anakunyuka. 3.Miguu katia ndani,myaka mitatu yafika Madili ya kibandani,yameanza sahulika. 4.Nalo joto la jioni,linazidi kutushika Posho zile vikaoni,nazo zimeadimika. 5.Na wanyonge kilioni,wengine wafurahika Kuipata ahueni,ile ilohitajika. 6.Ni mpingo wa porini,kwa shoka hutokatika Panga lako ni la nini,bure utaaibika. 7.Korosho za mashambani,ndo hivyo zinabebeka Ila zile za rohoni,mbali zaenda jizika. 8.Mze Baba yu vitani,magwanda yanavalika Kabeba debe la tani,na bakora kaishika. 9.Wale wavaa vidani,wameanza kuchizika Wanashanga vifuani,za dhahabu zatoweka. SHAIRI-MZEE BABA. MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha. +255624010160 iddyallyninga@gmail.com
1.Tulimponda fulani,kwamba anacheka cheka Kila siku yu angani,na madege anaruka. 2.Leo katua jamani,yule alofikirika Ukiuleta utani,ni fimbo anakunyuka. 3.Miguu katia ndani,myaka mitatu yafika Madili ya kibandani,yameanza sahulika. 4.Nalo joto la jioni,linazidi kutushika Posho zile vikaoni,nazo zimeadimika. 5.Na wanyonge kilioni,wengine wafurahika Kuipata ahueni,ile ilohitajika. 6.Ni mpingo wa porini,kwa shoka hutokatika Panga lako ni la nini,bure utaaibika. 7.Korosho za mashambani,ndo hivyo zinabebeka Ila zile za rohoni,mbali zaenda jizika. 8.Mze Baba yu vitani,magwanda yanavalika Kabeba debe la tani,na bakora kaishika. 9.Wale wavaa vidani,wameanza kuchizika Wanashanga vifuani,za dhahabu zatoweka. SHAIRI-MZEE BABA. MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha. +255624010160 iddyallyninga@gmail.com
swissme JF-Expert Member Joined Aug 15, 2013 Posts 13,663 Reaction score 19,906 Nov 13, 2018 #2 Swissme
Lyaka mlima Senior Member Joined Dec 21, 2017 Posts 140 Reaction score 83 Nov 13, 2018 #3 Shairi zuri