Miaka 500 ya Mapinduzi - Martin Luther

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838


​



Martini Luther! Niseme nini tena huyu ndiye Mwanamapinduzi, Mwanamageuzi wangu mkubwa aliyewahi kuishi Dunia hii!

Martini Luther aliyezaliwa huko nchi ya Ujerumani Bara la Ulaya, Mwaka 1517 alifanya Mapinduzi makubwa sana ndani ya Kanisa Katoliki, Mapinduzi hayo ndiyo yaliyopelekea kuzaliwa kwa uprotestanti Duniani hii!


Mwana mapinduzi huyu aliyepingana na Kanisa Katoliki la wakati huo kwenye mambo kadhaa hasa kuhusu stahili za matendo mema, hoja kuu ya Martini Luther ilikuwa ni kwamba alitaka Kanisa Katoliki libadilike na kuendeshwa kwa kufuata Mafundisho ya Yesu Kristo na Biblia jambo ambalo Papa alilipinga kwa nguvu zote jambo lililopeleka kutokea kwa vita kubwa na hatimaye kuanzishwa kwa Uprotestant!

Ieleweke ya kwamba Martini luther hakuwa na lengo la kutoka Kanisa katoliki bali alitaka kulibadilisha na kufwata Maandiko ya Yesu Kristo!
Martini Luther aliuliza maswali magumu sana kwa wakati huo, kwa mfano ni kwa nini Misa na mafundisho ya kidini yawe kwa lugha ya Kilatini na siyo Kijerumani lugha inayoeleweka na watu wake wote? Mungu anaelewa Lugha yoyote ile sasa ni kwanini waumini walazimishwe kuabudu kwa kutumia lugha ya kigeni (Kilatini)?

Maswali haya yalileta Mapinduzi Ulimwenguni kote kwani Martin Luther kinyume na matakwa ya Papa alitafsiri Biblia ktk Kilatini kwenda Kijerumani jambo ambalo liliigwa na wananchi wa nchi nyingine kama vile Waingereza nao wakatafsiri Biblia ktk Kilatini kwenda kwenye lugha yao King's James Bible na mpaka sisi pia leo hii tuna Biblia iliyoandikwa kwa Kiswahili hii yote matokeao ya kazi ya Mwanamapinduzi Martini Luther, bila Martin Luther si ajabu mpaka leo hii Biblia ingekuwa imeandikwa kilatini kama ilivyo kwenye Dini nyingine!

Kwangu mimi huyu Ni Mwanapinduzi anayefaa kuigwa na kutukuzwa siku zote hasa kwa kuonyesha Uthubutu wake!
Je Martin anatufundisha nini sisi kama watz ukiangalia changa moto tulizonazo? Je, Changamoto zetu kubwa klk Martini Luther alizokuwa nazo na tushindwe kujikwamua...

Nimetoa changamoto kwetu wakati Dunia inajitayarisha kuadhimisha miaka 500 ya Mabadiliko au ya uprotestanti, ingefaa na sisi tuige mfano wa Martin Luther tubadilishe hali mazoea tuliyonayo, inawezekana, hakuna kazi ngumu kama aliyokuwa Martin Luther kama aliweza hata sisi pia tunaweza kuichukua Nchi yetu ktk kwa Makupe na wanyonyaji na kuibadilisha kuwa nchi ya Haki na Usawa kwa watu wetu (Bila Wahindi Waarabu, Machotara, Wazungu &Co. ikiwezekana tuwanyang'anye Uraia)


Ikumbukwe ya kwamba pamoja na kupingwa kwake na Kanisa Katoliki, bado kanisa hilo hilo lilichukua baadhi ya mapendekezo yake na kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuruhusu Biblia kutafsiriwa kwenye lugha mbali mbali n.k hivyo hapo kuna mengi sana ya kujifunza kwetu sisi Watanzania kutoka kwa Martin!




Mahali ambapo Luther alitafsiri biblia ya kwanza ktk Kilatini kwenda Kijerumani, na Mapinduzi yalianzia hapa na kusambaa Dunia kote mpaka kwetu TanZania!



Biblia ya kwanza kutafsiriwa Duniani ktk Kilatini kwenda kwenye Lugha ya Martin Luther!


​
 

Attachments

  • 1280px-WartburgLutherstube1900.jpg
    147.1 KB · Views: 393
Kulikuwa na 27 bible edition in germany kabla Martin Luther hajatafsiri. Kusema Martin Luther ndio mtu wa kwanza kutafsiri Biblia ni uongo mkubwa pia. Agalo la kale liliandikwa kwa Kiebrania na kuja kutafsiriwa na wasomi wakijewish kwenda kwenye kigiriki karne za awali kabisa. Baadae St. James alitafsiri kwa Kilatin lugha iliyokuwa kubwa na maarufu wakati huo.
Anyway faida ya mapinduzi yake miaka 500 sasa tuna madhehebu ya Kikristo zaidi ya elfu 30...kila mmoja akijifanya mjuaji wa kutafsiri.....
 
Ila alienda mbali zaidi kwa kutaka baadhi ya vitabu viondolewe kama masadukayo na ufunuo wa yohana.
 

Labda basi haujaelewe nilichomaanisha ni hivi Hapo zamani huko Ulaya Biblia zote zilikuwa zimeandikwa kilatini, yaani Himaya ya Roma ilitafsiri Bibia ktk Kigiriki kwenda Kilatini na wakati huo Kilatni ndio kilikuwa lugha kuu ya Bara la Ulaya hivyo mafundisho yote ya kidini yalikuwa kwa kilatini, Na ni Martini Luther ndiyo aliyelipinga hili na kusema ni lazima Biblia itafsiriwe kwenye lugha mbalimbali ili watu wengi waweze kunufaika Papa alipinga lkn yeye alitafsiri ktk Kilatini kwenda Kijerumani na hayo yalikuwa ni mapinduzi mkubwa na wengine wote nao wakafwata na Ulaya nzima wakaanza kutafsiri Biblia ktk Kilatini kwenda kwenye lugha zao kwa kufwata mfano wa Martini Luther hivyo Biblia kama King's James na nyinginezo mpaka Kiswahili pia zikafwatia!

Kumbuka nimesema alikuwa wa kwanza kutafsiri Biblia ktk kwenye Kilatini kwenda kwenye lugha za Ulaya na hapa naongelea bara la Ulaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…