GE2025 Mgombea huyu wa CCM ni hatari ustawi kwa jimbo la Geita Mjini, amefoji vyeti

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

kono kono

New Member
Joined
Jul 25, 2025
Posts
1
Reaction score
1
Leo team ya Mgombea wa ubunge jimbo la Geita mjini mwenye kashfa ya kufoji Vyeti na kugawa Rushwa hovyo inashangiliwa baada ya kuhakikishiwa jina lake kurudi kwenye majina yatakayo Rudi kuwaania ubunge jimbo la Geita mujini, kijana huyo ambae amepofusha baadhi ya wajumbe kwa Rushwa leo ameonekana na Team yake kusherekea jina lake kurudi katika nyumba yake iliopo Tawi la bombambili kata ya Bombambili jimbo la Geita mjini.

Kwa Mujibu wa Biblia kutoka 23:8 inasema “Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki”. Mstari huu ndani ya Biblia umeonekana katika jimbo la Geita Mjini baada ya Mmoja wa mgombea ndani ya ccm (jina tunalo) amekuwa akigawa Rushwa hovyo hovyo bila hofu ili awe Mbunge wa jimbo la Geita mjini, kijana huyo ambaye pia amefoji cheti cha stashahada (Diploma) kutoka chuo Hulia cha Tanzania ili awe na CV pana kama wenzake.

Mgombea huyu ambaye kidato cha pili kutoka shule ya Sekongari ikizu alifeli amekumbwa na kashfa mara kadhaa ya kugawa Rushwa za Pikipiki, Simu na pesa kwa wajumbe na kujinasibu kuwa yeye hawezi kuchukuliwa hatua za kinadhamu kwa sababu anapesa, Mgombea huyo ambae ni kiongozi wa jumuiya ya uvccm hashikiki wala hakamatiki kwa sababu anatamani aingie bungeni ili mambo yake yanyokee.

Japo wananchi wanamuona bado akili zake hazijakomaa ila kwa sababu ya pesa anazotoa hata zezeta, anashinda kwa sababu wajumbe baadhi wameshapofuka kwa sababu ya Rushwa, amesema kwa hesabu ndogo ndogo mpaka sasa ameshatumia bilion 2 kwa kumalizia atatumia Bilioni 3 ili tu aingie Bungeni, kijana huyu walionyuma yake ni baadhi ya matajiri wa dhahabu wanataka wapate mtu ambae watakuwa wanamtuma anawafanyia kazi zao kama kutafuta leseni za uchimbaji.

Ameongea mmoja wa Mjumbe " Huyu dogo hafai maana leo ametualika kwenye sherehe ya kusherekea jina lake kuwemo kwenye kinyang'anyiro maana kuna mtu kamuhakikishia, hilo ajiandae tu" huyu kijana ambae amekuwa akiikanyaga kanuni za chama wazi wazi amekuwa anajiamini sana kuwa hawezi kukatwa yeye, pamoja na kufoji cheti chake na kutoa Rushwa hadharani bila kificho, karibuni tuone ambavyo Rushwa imewapufua wajumbe wa jimbo la Geita mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…