Mchepuko Niachie

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,265
Reaction score
4,453
Kwa huzuni naandika,Moyoni nahuzunika
Nikweli limenitokea,majuto ni mjukuu
Natamni rudi nyuma,Historia badilisha
Mchepuko niachie,Familia niijenge

Najua nilikosea,huba yako kuionja
Utamu nilinogewa,nikasahau wajibu
Penzi limetamalika,sasa nimekuwa Zoba
Mchepuko niachie,Familia niijenge

Kipato changu kidogo,kukutunza sitoweza
Majukumu yamebana.nahisi kutokwa roho
Natamani kula vyote,mfuko hauruhusu
Mchepuko niachilie,Familia niijenge

Kiuno chako cha nyigu,Na sura yako ya yai,
Ngozi yako yateleza,manukato yalewesha
Mavazi yako murua,si mtumba si spesho
Mchepuko niachilie,Familia niijenge

Maliwato mejaliwa,mbinukowo mwanana
Nikiushusha mkono,watulia palepale
Kiunocho ni chembamba,Namba nane yajichora
Mchepuko niachilie,familia niijenge

Kunako sitakwasita,bidiiyo naiona
Unanitoa utamu,kwa kweli unajituma
Mahabayo ni adimu,hakika umehitimu
mchepuko niachilie,familia niijenge

mdekewo wa pekee,walia kila sauti,
mara 'bebi' mar hani, yaani unanidatisha
Kama mahaba maradhi,basi mimi mahututi
mchepuko niachilie.familia niijenge

Mkasa umenikumba,kwa sasa ni njia panda
Mchepuko unang'ang'ana,wataka daima dumu
Mwenzenu nataka toka,nirudi kwa mke wangu
mchepuko niachie,familia niijenge

Makosa nilishakosa,Utamu nshaonjeshwa
Mitara sitoiweza,mmoja ananitosha
Kuchepuka si ujanja,Ila kwa sasa najuta
Mchepuko niachie,familia niijenge

Malenga nawauliza,nifanye nini mwenzeni
Mchepuko umegoma,wataka daima dumu
Nataka nihame mji kukimbia mchepuko
mchepuko nichilie,familia niijenge

Tamati nimefikia,mkasa bado kuisha,
bado nipo majangani,hali yangu napambana
Natamani jua suluhu,ya hili langu janga
Mchepuko niachie,familia niijenge

PBK
 
ngoja wako njiani
 
Ushairi wa maana... Naamini atakuelewa mkuu
 
Tungo nzuri sana masikioni kusikia,
Heko kwako mtunzi ujumbe kutufikia,

Mchepuko utoe nduki malengo kufikia....
 
Haki mtunzi uko vzr mm nimependa
 
Shairi lla kufa mtu...Hongera kama hata halitaeleweka kwa wengine, keep it up...
 
Ushairi huu nimeupenda sana kwa kweli, michepuko mtuache 2018 tujenge familia.
 
Safi sana mimi umeshaniacha kwa shairi hili dah maana ulinikomalia ila baada ya kumpa hili shairi alisome tu kaelewa
 
Uliyeandika hili shairi ukikamatwa utafungwa.
Shairi lako limekosa mizani na vina.
Umetumia maneno matamu na ya kupendeza na ujumbe ni maridhawa ila umevunja kanuni za ushairi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…