Nimelala nimekesha, jambo nimefikira Bongo nimezichemsha, sipati jibu sawia Hivi kweli Umekwisha Uzalendo Tanzania? Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
Ona walivyoziuza, rasilimali za mtanzania Kwa kweli inashangaza, mikataba waloingia Kisha tukiwauliza, hawana la kutwambia Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
Rushwa imekuwa ngao, kumdhulumu raia Ubinafsi kwao nguo, vazi la kujivunia Hizi ndizo sera zao, katu hawajui njia Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
Wananchi amkeni, haki kujitafutia Mtalala mpaka lini?, saa imeishawadia Uwongo ukataeni Waache kuwatania Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
Mkipiga kura zenu, chagueni mwenye nia Waonesheni wanenu, muelekeo na njia Fanyeni vitu vyenu, tuiokoe Tanzania. Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania
Mchagueni Slaa, kiboko cha Mafisadi Huyu bwana hana njaa, atatwanga wakaidi Ni kiongozi shujaa, si mtumwa wa itikadi Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania