Maziwa yananipa shida

kibenten

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
499
Reaction score
511
Habari wakuu.

Nimekuwa nikinywa maziwa fresh tumbo linajaa gesi nakuwa najamba jamba ovyo tu,,hali hii ilikuwa hainitokei hapo kabla nilikuwa nakunywa maziwa mabichi baada tu ya kuyakamua kutoka ngombe wangu wa kienyeji na kuyanywa apo apo na nlikuwa sipati shida yoyote.

Ila saiv nikinywa tumbo linajaa gesi nilaunguruma kutwa nzima na mda mwingne kutaka kuharisha kabisa.


TATIZO NINI ?
 
Sasa si uendelee kunywa hayo hayo mabichi?

Kuna watu wa vijijini wakija town wakinywa maji yaliyochemshwa wanaumwa tumbo,lkn wakigonga Yale maji Yao ya mtoni fresh tu wanadunda.
 
Kuna watu ni kweli inawatokea..wanapata kitu kinachofanana na GERD(Gastroesophageal reflux disease).

Sema inabidi upunguze kiasi unachokunywa day by day baada ya muda ukinywa mengi utakaa sawa tu.
 
Kuna watu ni kweli inawatokea..wanapata kitu kinachofanana na GERD(Gastroesophageal reflux disease).

Sema inabidi upunguze kiasi unachokunywa day by day baada ya muda ukinywa mengi utakaa sawa tu.
mbona zamani nlikuwa nakunywa hata lita mbili na ni kila siku,afu nlikuwa sipati tatizo lolote?
 
Wewe ni miongoni mwa watu wenye tatizo la "lactose intolerance"

Hivyo maziwa huyawezi ni bora ukaacha kunywa
mbona zamani nlikuwa nakunywa hata lita mbili na ni kila siku,afu nlikuwa sipati tatizo lolote?

nmekunywa maziwa toka nazaliwa hadi saivi, lakini hizi siku za karibuni ndo yameanza kunipa shida (almost kama miezi minne sasa hili tatizo limeanza)
 
Pole ila kunywa maziwa mabichi kunahitaji moyo, kwangu mm siwezi
 
mbona zamani nlikuwa nakunywa hata lita mbili na ni kila siku,afu nlikuwa sipati tatizo lolote?

nmekunywa maziwa toka nazaliwa hadi saivi, lakini hizi siku za karibuni ndo yameanza kunipa shida (almost kama miezi minne sasa hili tatizo limeanza)
Kadri umri unasonga tatizo la "lactose intolerance" huwa linaongezeka. Na hii shida inawapata zaidi waafrica kuliko wazungu. Ni tafiti zinasema hivyo. Inawezekana na ww una hiyo shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…