Wakuu habari za majukumu,
Nimekuwa nasumbuliwa kwa muda marefu na maumivu ya shingo upande wa kushoto na kichwa kwa muda mrefu. Desemba 2019 nikaumwa sana sikio la kushoto pamoja na Koo. Nikahisi nina vidonda vya koo na uambukizo wa sikio. ENT Specialist akasema sina tatizo lolote katika maeneo hayo na kunishauri niende kwa Dentist.
Matokeo ya kwenda kwa Dentist ni kama picha nilio ambatanisha hapa inavyoonyesha.
Dentist alinipa madawa antibiotics na pains killers baada ya kuyasafisha. Lakini tatizo bado lipo na jino linauma sana hasa kwa ndani kwenye fizi.
Naombeni ushauri wenu wataalam wa humu JF.
View attachment 1402430
Sent using
Jamii Forums mobile app