Maulid Mtulia ni mbunge pekee wa UKAWA aliyeshuhudia kuapishwa kwa viti maalum wa Lipumba

Biblia imeandika au imeandikwa?
Biblia yenyewe haiandiki, rekebisha kwanza lugha
Kuna masahihisho mengine yanaonesha zaidi "mediocrity" yako kuliko kukosa umakini kwa mwandishi. hiyo nukuu ni nzito sana lakini umeamua "kuchuja mbu", kama asemavyo Bwana Yesu katika hiyo hiyo Biblia, "viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia" [Mathayo 23:24].
 
Umenikumbusha Dr Slaa alivyokuwa akilipwa stahiki za kibunge na chama chake ilhali yeye si mbunge akapewa " cheo" cha mgombea wa uRais!
Ilikuuma sana eeh? lakini ile ni tofauti sana na hii. Yule aliacha yote ili awakilishe chama chake katika kugombea urais, katika kujitoa zaidi kwa chama chake. Yule (Dr Slaa wakati ule) alizawadiwa na chama chake mwenyewe kama kifuta jasho kwa kujitoa kwake, huyu kahongwa na chama cha mafisadi (CCM) ili akitose chama chake. Ya Dr Slaa wakati ule yalitangazwa hadharani, ya huyu kwa kuwa ni rushwa, yanafichwa, ila yananuka sana maana unajiuliza mtu anaachaje alichopigania kwa gharama kubwa ya fedha, muda na jitihada, kienyeji tu? La Mtulia na la Dr Slaa wakati ule, tofauti yake ni usiku na giza. ila kama umefaulu kuyaunganisha, basi unastahili kutunukiwa nafasi katika chuo kinachoitwa "Milembe Hospital"
 
Ndo maana nasema siku zote sitakujafanya upumbavu wa kupiga kura, nikupoteza muda tu. Mtu akitaka kugombea nafasi yoyote ya kisiasa achukue mke wake watoto wake na ndugu zake ndo wakampigie kura, sasa wewe jitie kiherehere ukapange foleni masaa matatu au matano upige kura kisha unaemchagua akuletee utumbo na katiba hairuhusu kumuwajibisha na kuuazibu.
 
Kabisa
 
Hahahaa......... hakuna tofauti yoyote kwani Chadema wana chanzo gani cha fedha zaidi ya ruzuku ambayo ni kodi ya wananchi?!!
 
Mkuu yani wakazi wa kinondoni wanatukana sana kitendo cha bwana mtulia kuwavua nguo na wanasema hawakulala siku tatu kumpigania ubunge ila yeye katumia dakika moja kuwaacha tupu.
Huyu jamaa alikuwa anakubalika nakumbuka fika kipindi cha uchaguzi nilikuwa kino hata matokeo yalivyokuwa yanacheleweshwa watu walijua anaibiwa mpaka mabomu yalirushwa

Jamaa kazingua sana
 
Hahahaa......... hakuna tofauti yoyote kwani Chadema wana chanzo gani cha fedha zaidi ya ruzuku ambayo ni kodi ya wananchi?!!
Sidhani kama kuna chama kinategemea ruzuku tu. ingekuwa hivyo vile vyama ambavyo havina ruzuku vingeshakufa siku nyingi. lakini pia CCM pamoja na kujichotea fedha watakavyo toka hazina, bado wanategemea fedha kutoka vyanzo vingine: wafadhili toka ndani na nje, kadi na viingilio, nk.
 
Kulikuwa na makubaliano ya UKAWA kutoka nje ya bunge ili kuonyesha kupinga kwa vitendo kusiginwa kwa katiba ya Tanzania kuhusu namna majina ya mfukoni mwa Lipumba yalivyoletwa na kuapishwa bungeni
Ukawa ilishakufa mara tu baada ya lowassa kujiunga na chadema
Ndio maana uchaguzi wa madiwani mliopata kata 1,hatukuwahi kusikia msamiati huo
 
Hiki kitendo kina tofauti gani na kile alichofanya Nyarandu?
 
Hiki kitendo kina tofauti gani na kile alichofanya Nyarandu?
 
Hata kwa nyalandu ingekuwa hivohivo, tazama pande zote mkuu, kwani mpaka sasa ni ngoma droo huku nyarafu huku mtulia
 
Sababu za Nyalandu zimeungwa mkono na wananchi , za Maulid zimepingwa vibaya sana ! Nashauri aongezewe ulinzi .
Hata za mtulia zimeungwa mkono vilevile, kama ni ulinzi mbona hamkuweka kwa nyarandu lowasa aumaye na wengine
 
Sababu za Nyalandu zimeungwa mkono na wananchi , za Maulid zimepingwa vibaya sana ! Nashauri aongezewe ulinzi .
Sababu za Wema nazo zilipingwa vibaya na 'wananchi' (ambao kwa definition yako = wapinzani) pamoja na mama yake mzazi. Kwa hiyo naye aongezewe ulinzi? Kwani hao 'wananchi' huwa wanawafanyaje kama hawakuongezewa ulinzi?
 
Sababu za Wema nazo zilipingwa vibaya na 'wananchi' (ambao kwa definition yako = wapinzani) pamoja na mama yake mzazi. Kwa hiyo naye aongezewe ulinzi? Kwani hao 'wananchi' huwa wanawafanyaje kama hawakuongezewa ulinzi?
Wema alikuwa mbunge wa jimbo gani ? Hivi unafahamu jinsi huyo Mamluki Mtulia alivyoupata ubunge wa Kinondoni ? Tema mate chini mkuu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…