Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Wabunge Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza mchakato wa kusajiliwa Jijini Dodoma.

Majina yao yamewasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA

ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA 2020:
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed

HOTUBA FUPI YA HALIMA MDEE KWA NIABA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA

Mheshimiwa spika, nitazungumza kwa niaba ya wenzangu wote kwa hiyo nitazungumza peke yangu. La kwanza nikushkuru kwa amabo umepelekea kiapo kikafanyika

Pili nikishkuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kwasababu kupitia wao ndio sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu ambacho kwa mujibu wa matakwa ya sheria za nchi kimekidhi vigezo vya kupata viti maalum, kwa hiyo viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.

Nikuhakikishie mheshimiwa spika na mimi unanifahamu vizuri, tumefanya kazi wote kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile ambavyo tumekuwa tukivifanya.

Lakini mwisho lakini sio kwa umuhimu, tuwahakikishie vile vile watumishi wa Bunge, kuna vijana wapya hapa wameingia, sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi bora na nzuri kwa ajili ya Taifa hili.

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana. Baada ya kusema maneno hayo Mh Spika nirudie kukushkuru wewe, katibu wa Bunge na timu yake wewe na nikishkuru chama chetu kwa sababu kupitia

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu ndio tumepata fursa hii ya kuwakilisha watu wengi ambao wana imani na sisi.

SPIKA NDUGAI: Muongezeeni makofi Halima, ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wapya na kwa niaba yenu wote ningeomba tuwapigie makofi.

Kwa mujibu wa ibara ya 78, ibara ndogo ya kwanza ikisomwa na ibara ya 66, ibara ndogo ya 1(B) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Vyama vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge vitapendekeza kwa tume ya Taifa ya uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa wabunge ili hao waliopendekezwa wawe wabunge wa viti maalum kupitia vyama hivyo.

Tarehe 20 Novemba 2020 nimepokea barua kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi yenye maelezo kuwa imefanya uteuzi wa wabunge wanawake 19 wa viti maalum wa CHADEMA kwa mwaka 2020 ambao ni kama tulivyowaapisha hapa.

Mimi kama spika nawaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ni ya wabunge wachache, wajibu mmojawapo wa spika ni kuwalinda wale walio wachache, nitajitahidi sana kuwalinda, nitajitahidi kuwapa haki, nitajitahidi kuhakikisha kwamba mnatekeleza majukumu yenu kikamilifu katika kuwatetea watanzania, kuwasemea watanzania na kufanya kila lile ambalo linawapasa katika kazi za kibunge ili muweze kufanikisha jukumu hili la kikatiba.




Viti.jpg

Bunge.jpg

Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) wakiwa na Spika Ndugai

Suala hili lilizungumziwa na mwanaJF hapa > Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na wanawake wa CHADEMA

CHADEMA yakanusha kupeleka majina > John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum, tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua
 
Kidogo tuu wametepeta? Kwa kweli inatia hasira, tena wamuombe radhi yule mbunge wao dada wa Nkasi waliokuwa wanamkataza kuapishwa. Tena ina maana wamem snitch hata Lissu aliye utangazia ulimwengu kuwa katu CHADEMA hatutashiriki kwenye shughuli za Bunge na walla hatuitambui serikali iliyoingia madarakani kimizengwe?
 
Back
Top Bottom