Nadhani unayo hoja ya msingi kabisa. Ila kukufumbua macho zaidi ni vema ukafahamu kuwa ndoa haijawai wala haitawahi kuja kuwa outdated concept bali shida ni wahusika wanaoingia ndani ya ndoa kutokuwa na vigezo au uwezo wa kusimama ndani ya ndoa.
Kuna sababu ambazo kimsingi zinasababisha ndoa katika kizazi cha sasa kuwa kazi kubwa kuitumikia, na sababu zenyewe ni kama ifuatavyo:
1. Ndoa ni taasisi, na kila taasisi ndani yake ina watendaji wenye vigezo na uwezo wa kuitumikia. Huwezi kuajiri askari jeshi bila mafunzo ya jeshi. Huwezi ajiri muhasibu bila kufuzu mafunzo ya chuo na CPA, huwezi ajiri mkemia bila kuwa na cheti cha mkemia, je kwenye ndoa, hawa mabinti wa kisasa na vijana ni wapi hukaa kambi hata ya mwaka m'moja kupitia mafunzo makali ya ndoa?
2. Wanaume wameshusha sana standards zao kwa wanawake na wanawake wamepandisha sana standards zao kwa wanaume. Mwanamke zamani aliqualify kuwa mke kwa kuwa bikra kama sifa ya lazima, halafu tabia nzuri ikawekwa kama sifa inayofuata ya lazima.
Leo hii wanaume hii sifa hamuhangaiki nayo tena wanaume wengine wanatetea kabisa kwa kusema kwan kuna ubaya gani akiwa hana bikra, hawa ni wanaume wanaotetea si wanawake, sasa kwann wanawake wasikubaliane na huo uhalisia kuwa wanaume hawana shida na bikra watatuoa hata wakikuta tulishazaa na wanaume kwahiyo wacha tukachezewe kuna mabwege yatatulipia mahari na kutuoa.
3. Wanaume miaka hii wamekuwa wakwepa majukumu au wabeba majukumu yasiyowahusu. Mwanaume anazaa na binti ila hajui wajibu wake kama Mume na baba, hajui majukumu yake kwa kitu alichokianzisha mwenyewe anatoa toa macho kama ng'ombe na kusubiria wakwe, mashemeji, na familia yake wafanye jambo kumsaidia. Au anakutana na mwanamke ambaye sio wake ana watoto yeye huyo kabebelea, ni wa kwako? Kwann usitafute wa kwako? Hiyo roho nzuri si ungelea watoto wa dungu zako wenye hali ngumu, kwenda kulea mabao ya watu halafu ndio uitwe mwanaume wa shoka ni ujinga kutoka sayari gani huo?
Kwa sampuli hii ya wanaume ndoa haiwezi kuwa imara.
4. Kudharau mafunzo ya kimaadili na Maagizo ya mwenyezi MUNGU ambayo kaagiza watu kuyafuata ili kuwa imara kiimani na kimwili ila viburi sasa vya wanadamu leo ndio matokeo yake tupo hapa ndoa zinaendeshwa kwa idea za movies za Hollywood, tamthiria za Telemundo, na hawa relationship coaches wa mitandaoni.
5. Wanawake wa sasa ni wavivu eneo la ndoa ila wanabidii kujihangaikia. Mwanamke unaweza mkuta alikuwa amepanga analipa Kodi kwa biashara ndogo ndogo au ameajiriwa lakini siku ukianza kaa nae ndani hatochangia hata 1000 endapo kutakuwa na dharula na mwanaume haupo karibu au haupo na vema kiuchumi kwa kukwambia wewe ni mwanaume as if yeye ndie huwa analipa 100% ya bills. Kwa kifupi ubinafsi.
So kimsingi Ndoa haijawai na haitakuja kuwa outdated concept shida ni wahusika kutokutambua na kusimamia vigezo vya ndoa na kuisimamia vilivyo kwa kila mojawapo kukaa eneo lake na si kuingiliana.