Basi mimi l got it all wrong, maana nilifikiri wanaojipenda sana huwa wanawachukia wengine, maana huwa so selfish and unconsiderable.
And hence your question is??- Mwanadamu anajipenda nafsi yake
- Mwanadamu anapompenda mwanadamu mwingine ni mwendelezo wa kujipenda nafsi yake mwenyewe
- Mwanadamu anapomwagwa, anapokataliwa ama anapoacha kupendwa na mwenzake huishia kujichukia
- Mwanadamu anapojichukua basi mwisho wake ni kuvuka mstari na kumchukia yule aliyekuwa anampenda
*Dhana ya kumpenda mwanadamu mwingine kama nafsi yako haipingani na hii mantiki ya mstari mwembamba
English translation to follow shortly, oops, I mean later!
lol, huwezi kumpenda binadamu mwingine kama hujipendi, tena watu wasiojipenda ni wagumu sana kwenye mahusiano maana wanajaribu kulazimisha wapendwe sana ili kufidia ombwe zito walilo nalo moyoni kwa kushindwa kujipenda nafsi.
Companero
Kuna simulizi maarufu sana ya MSAMARIA, nina uhakika unaielewa.
Tunasimuliwa kuwa Msamaria alimsaidia yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi, akamfanyia huduma ya kwanza na kumpeleka Hospitali na kumlipia gharama, na akaagiza kuwa kama kungekuwa na ziada basi angekuja ku-clear wakati akirudi toka huko alikokuwa akienda!
Huyu mtu kwa kitendo chake cha kumpenda mtu asiyemjua na kumsaidia, anaendelezaje himaya ya kujipenda mwenyewe?
Huoni kwamba hii inapinga dhana yako?
nakubaliana na Kaunga ,watu wanaojipenda sana huwa selfish na hawawezi kutoa upendo huohuo kwa wenzao,instead inakuwa its all about wao yan wao wanaona wanastahil kupendwa ila hawapaswi kutoa kwa kipimo kilekile!
PakaJimmy bado kuna upendo wa kristu hadi akakubali kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine. Sasa siamini mtu anayejipenda anawezaje kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine.
Biblia inaassume kila mtu ni selfish Fulani (anayejipenda) na ndio maana inawashawishi watu wawapende wenzao kwa kipimo hicho hicho wanachojipenda. Sasa kama kweli kila mtu anajipenda, basi hakuna mtu angemchukia mwenzake kwakuwa kigezo cha kumpenda mtu ni kuweza kujipenda wewe.
Mimi ninafikiri wanaojipenda wenyewe sana, they are very weak n insecure inside au wanakosa upendo ndio maana wanatumia nguvu nyingi sana kujipenda.
Compareno,
Hii mada yako inanirudisha moja kwa moja katika makala ya juzi ya BBC kuhusu "Narcissism" iliyozungumzia Freud "His Majesty The Baby" concept, mythology ya Kigiriki ya Narcissus na kanuni ya kwenye biblia ya "Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako"
Kuna uhusiano wowote au ni coincidence tu inayotokana na ile dhana ya "great minds think alike"?
Kama ni katika kuwasilisha dhana ile ile ya kwenye makala, basi lazima ikuwie vigumu kwa sababu hatuna neno linalofanana kimaana na narcissist kwa kuanzia
lol, ni coincidence tu. hiyo programu ya bbc sijaiona.freud nimemsoma zamani sana.na biblia sijaifungua kwa muda (niombee kuhusu hilo).hizi ni tafakuri zangu za alfajiri nikiwa kitandani baada ya kuamka.
Good for you @ tafakari za alfajiri.
Lazima mapinduzi ya fikira yapatikane kwenye jamii ya Kitanzania mwaka huu, manake alfajiri tu tafakuri hizi, jee ikifika jioni?!
*Kwani na programu yake ilitoka? Mie nilikuwa nazungumzia makala