mambo ya urithi

don makup

Member
Joined
Oct 3, 2016
Posts
7
Reaction score
6
Mimi nimefiwa na mzazi ( baba) mwezi wa pili mwaka huu 2016. Watoto tupo nane. Yaani kuna kaka wa kwanza ni wa nje yaani baba alizaa nje ya ndoa. Then kuna madada wawili baba aliwakuta kwa.mama. Then kuna kaka yangu nje ya ndoa ila mama moja. Then kuna mimi ndani ya ndoa ( male). Then kuna mdogo wangu mama mwingine. Then kuna wadogo wawili wa kike mama mwingine. Sasa mimi mama yangu.mzazi walitengana na baba uangu kama miaka 25 iliyopita ila si mahakamani walikubaliana tuu ki utu uzima. Akaondoka na dada zangu tukabaki wanaume watatu kwa baba. Badae kaka yangu mkubwa ( mama mwingine) alifukuzwa nyumbani kwani alikua mwizi na hata mzee kumfunga gereza la kinguruwila mwaka moja. Sasa baada ya baba kufa mama yangu mzazi alimkabithi usimamizi wa mirathi huyo kaka mkubwa kwa kuogopa baada ya kuona alianzisha vurugu. Sasa toka mzee amefariki hakuna kikao kilichofanywa na hakuna mawasiliano toka kwa msimamizi wa mirathi ( huyo kaka wa nje). Mimi naishi nje ya nchi. Je ushauri wa kisheria ama mawazo naombeni mnipe. Hiyo blaza kauwezo anako na ni mzoefu shule ya kitaa dar es salaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…