Yajue mambo matatu yanayojenga UPENDO zaidi baina ya watu wawili wanaopendana:
1. Kujitoa
Hali ya kujitoa inapelekea kua na uwiano baina yenu mkapendana zaidi. Kujitoa ni ile hali ya kuwa na ushirikiano mzuri baina yenu.
Mfano rahisi: Mwanamke anaweza akawa anafua na Mwanaume akawa anamsaidia Mwanamke kuanika nguo au Mwanaume anafua huku mwanamke anamsaidia kuanika nguo.
2. Ukweli na Uwazi
Kua wakweli na wawazi baina yenu mkiwa mpo kwenye mahusiano kunawajengea hali ya kuaminiana. Ukweli na uwazi ni pamoja na kusikilizana maana mnapojijengea tabia ya kusikilizana inapelekea hali ya kuaminiana zaidi kati yako na yule umpendae.
3. Dhati ya Penzi
Unapoingia au unapochagua kuingia kwenye mahusiano usiingie kwa sababu fulani yupo kwenye mahusiano kwa hio ukataka kujionyesha na wewe kua una Mpenzi kitu ambacho sio kizuri.
Unapoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi yakupasa wewe ndie ambae umeridhia kwa MOYO mmoja kua kwenye mahusiano hayo.
Mfano rahisi: Wanawake wengi siku hizi wanaolewa pasipokua na Mapenzi ya dhati ila ukiwauliza kwanini wameamua kuolewa watakujibu kua walikua wanaitaka Ndoa.
Ila pia inakupasa utambue ya kwamba mwanamke akipenda hua anapenda pasipokua na shaka au majuto yoyote.
Unapoingia kwenye mahusiano hakikisha MOYO wako umeridhia kwa dhati kua na mwanaume / mwanamke ulienae. Usiingie kwenye mahusiano kwa kuiga au kwa kumuonyesha MTU fulani kua na wewe upo kwenye mahusiano.