mama mkwe pasua kichwa jamani

golden girl

Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
66
Reaction score
2
ndugu wana jf.ushauri wenu tafadhali, nilikuwa na mpenzi ambaye alinitambulisha kwao, lakini tulikuja kuachana yeye akaoa na mimi natarajia kuolewa next week. tatizo ni mama mzazi wa huyo ex wangu, naishi naye jirani hivyo mara nyingi napita kumsalimia lakini akiniona tu lazima aniombe pesa.na ikitokea sijapita atanibip sana,nikimpigia anaomba vocha ya kujiunga kabaang ya mwezi mzima,nikipita na hand bag anaitaka, nikipita bila kitu mkononi ananiomba viatu nilivyo vaa. nimekuwa nikimpa kila anachoniomba mpaka sasa nimechoka vilevile namuonea aibu. nifanye nini jamani naogopa kumjibu dry mana namuheshim sana.naombeni ushauri jamani
 
mh! na kwanini akuombe wewe asimuombe huyo mkwewe mwingine, umeshamtaarifu ex wako juu ya hilo km bado mwambie na umueleze kuwa ushaichoka hiyo tabia ya mama yk, coz ww binafsi washindwa kumwambia ex mkweo
 
mnhh mtu kukuomba unachokitumia kama nguo uliyo ivaa
ndo 'uchawi wenyewe huo'
una entartain vipi 'wanga' kama hao?
Kama huyo mkwe wake ni mfipa au mhangaza ajue amekwisha, hao wakiwa na nguo yako uliyowahi kuvaa wanakuwa tayari na data zako zote, infact wao ni windows 8. Huyo mama anamfunga binti wa watu aiolewe kwingine
 
Shida kaikuza mwenyewe kelele alete Jf!!!!!
Endelea kumpa tu mama mkwe wako
 
Ukitaka kumuua nyani usimtazame usoni!!!
 
unajiendekeza kumwogopa huyo mama
kwani ukimyima atakufanya nini?
watanzania tuache uoga usio na maana
mwanae ni X wako and she has no right whatsoever kukuomba kitu chochote kile.
Kuwa makini sana kuna kitu anakitafuta kwako.
jali mambo yako usiogope atakuonaje kwani yeye ndo mama mzazi?
 
Dada Shikamoo Mama Huruma, naomba na mimi uniunge Mini Kabaang.ntakutumia namba angu kwa pm/(eneo la siri)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…