Kamchumbia wa nini? Mie nilidhani uchumba maanake yake, maandalizi ya kuja kukuoa,au?
Imenibidi nisome upya thread,nadhani neno ndoa lina maana tofauti vichwani mwetu.Mfano baba anaamini ndoa ni mpaka waende kwenye nyumba ya ibada au mkuu wa wilaya au kwa kiongozi wa mila na hii ndo tafsiri ya wengi!
Wakati kiserikali kuna kitu kinaitwa "common law marriage" nayo ni ndoa tosha inayotambulika kisheria.
Kiranga nimekuelewa,kuhusu neno "kuoa" au "kuolewa" wewe unalitafsiri vipi?Kuhusu mwanamke kutokuacha nafikiri hiyo inatokana na imani fulani,sidhani kama tunaweza lizungumzia hapa.Hayo maneno ya kiswahili bado sijaona ubaya wake,tatizo tunayachukulia kutokana na dhana ya mwanamke kutokutoa talaka ambayo kama nilivyosema ni dhana ya imani fulani tena moja tu.Kwenye mfumo dume hapo napo kuna mkanganyiko.Mwanaume na mambo ya kiume.Mwanamke na mambo ya kike.Tukubali kuwa mwanamke anapoambiwa "acha kufanya mambo ya kiume" ni sifa?Sidhani,pia mwanaume anapoambiwa acha mambo ya kike,sio aibu.Unapoyataja mambo ya kikekike wewe ndie unaamua yawe tusi,kashfa au vinginevyo.Tafsiri iliyoko kichwani mwako.Lakini pia huu mfumo unaoitwa dume una mambo mengi lakini mengi zaidi yapo vichwani mwetu zaidi,sio halisi!
Una introduce kitu kigeni kabisa ambacho mie sijakiongelea halafu unakiunganisha tu kama vile nimesema kwamba wanawake wanapenda kuchupachupa.
Mie sijasema kwamba wanawake wanapenda kuchupachupa, nimesema mfumodume unasifia wanaume kuchupachupa (urijali, kiwembe etc) lakini hapo hapo unadharau umalaya huo huo kwa mwanamke (mama huruma, jamvi la wageni etc)
Mtu akiisema hii double standard ya mfumodume hamaanishi kwamba wanawake wanao"chupachupa" wanapenda kufanya hivyo.
Hii kilatini inaitwa "Non sequitur", it does not follow, umeunganisha vitu viwili ambavyo havina uhusiano, out of nowhere.
ukisema "stable relations out of marriage lazima itakuwa na flaws chungu mzima, tayari umeshaji contradict.
Halafu "stable marriage nje ya ndowa" ni kitu gani?
Bottom line, kuna mapenzi yanayostawi nje na ndani ya ndoa, ndoa si kitu kibaya wala kizuri. Kama unaweza kustawisha mapenzi bila ndoa, ndoa si lazima.
Kuna watu wamekaa bila ndoa miaka kibao, wameishi vizuri tu. Kwa pressure wakaamua kuoana, baada ya kuoana wamedumu miaka miwili tu.Talaka.
ndoa ni kama kukaa ndani ya nyumba mliyofungiwa. Hamuwezi kutoka mpaka mvunje milango (talaka) jambo ambalo litaleta kelele na bughudha (aibu kwa jamii, bado tuna stigmatize talaka). Kwa hiyo hata hao wanaodumu katika ndoa hatujui kama wanadumu kwa mapenzi ya kweli au kwa sababu wanakwepa aibu tu ya kuachana.
Watu wanaoamua kukaa wenyewe kwa kuelewana bila ndoa wanaweza kusema wanapendana kikweli bila kushurutishwa na ndoa. Ni kama watu walioamua kukaa pamoja ndani ya nyumba huku milango ikiwa wazi. kila mmoja ana uwezo wa kuondoka bila kuvunja mlango, lakini haamui kufanya hivyo kwa sababu anapenda kuwa pamoja na mwenzake.
Mi nadhani,kwa mtazamo wangu,hatujui ndoa ni nini,tafsiri mbovu za kidini ndo zinaleta shida hapa.Kukifuata kitu kimkumbo ni tatizo kubwa.Niliwahi kuanzisha mada siku moja hapa nikitaka kila mmoja aeleze ndoa ni nini,majibu yaliyotoka yanachekesha.Watu wanafungwa na dhana zaidi kuliko kitu halisi.Umapokuwa kwenye mahusiano nje ya ndoa mnaishi muda mrefu kwa sababu mnajiongoza wenyewe,kwenye ndoa tatizo mnataka muongozwe na dhana zaidi ya nyie wenyewe.Ndo maana mtu anakua mwaminifu nje ya ndoa,akiingia kwenye ndoa mambo yanabadilika![/QUOTE
Inawezekana kila mtu anataka namna yake ya ndowa lakini kwa ukweli hakuna asiejuwa maana ya ndowa. Ndowa uskitaka utaihusanisha na dini na isipotaka basi dini haihusiki. Kwa ufupi ni kuwa ndowa ni mfumo wa uhusiano unaokubalika na jamii. Sasa tafuta njia utakayoifanya isikubaliwe na jamii iwe ndowa.
Fikira kuwa ndowa ni kitu mteremko ni fikira potofu kwani hata huo uhusiano utakaofanya nje ya ndowa utakuwa na misukosuko yake na laiti kama hauuwezi kuwa na misukosuko kuna kitu gani cha zaidi iwapo mtafunga ndowa kitakacholetw tatizo?
Kiranga, Ex spika aliposema "acha wivu wa kike" alimaanisha kuna wivu wa kike na wivu wa kiume,hakuwa na maana wivu ni jambo la kike.But sisemi alikuwa sahihi kusema hivyo ila nimerekebisha kauli yako kuhusu ex spika.Niliposema mfumo dume una mambo mengi yaliyo vichwani mwetu ninamaana kuwa kwanza dhana yenyewe haijaanzia kwetu,imeletwa,lakini haina maana ni mbaya kwa msingi huo.Cha msingi inazungumzia mambo ya msingi ama la.Mambo yaliyo vichwani ni kama tafsiri ya kuoa na kuolewa,hiyo tafsiri ya kumilikiwa imetokana na tafsiri ya kidini ambayo haiko sahihi.Naamini kuoa sio mbaya ubaya ni tafsiri tuliyowekewa vichwani.Mfano nikikuambia hakuna sehem za siri kwenye mwili wako unaweza ukanishangaa.Ni kawaida si umeambiwa zipo?Lakini hii haina maana dhana ya mfumo dume haina maana.Kuna mambo kama mwanamke kutokua kiongozi ni mambo ya ukweli ya kimfumo dume.Ila sijasikia hawa wanaodai haki za wanawake wakipinga viti maalum kwaajili ya wanawake pamoja na kupewa max za chini kwenye ufaulu.Mwanamke apewe viti maalum bungeni kwa sababu gani?Huku ni kumwaminisha kuwa yeye ni dhaifu.Unampa upendeleo wa ufaulu kwa nini?Hii sio HAKI!
Ungetaka kuishi kama jamii static usingekuwa kwenye internet sasa hivi wewe, kwani jamii yetu ndiyo iliyovumbua umeme, computer na internet?
Swala si jambo limeanzia wapi, swala ni je, linafaa au halifai?
Hizi habari za kutukuza sana a failing othodoxy zinatufaa au hazitufai?
Utakuta mtu kwao masikini hajiwezi hali wala mali, na yeye anachangisha masikini wenzake kibaooo wenye majukumu kemkem, bora hata kama angekuwa anawachangisha kujenga nyumba tungejua anafanya la maana.
Kumbe muharusi mkuuubwa.
Halafu baada ya harusi wanaingia kwenye chumba cha kupanga, hata zawadi walizonunuliwa hawana pa kuziweka.
Baada ya miaka miwili talaka.
Hivyo hiyo akili?
Kati ya huyo na anayefuatisha mapenzi ya kweli yasiyo na kelele za miharusi wala ndoa za kuapishana nani afadhali?
Naona hujauliza hizo flaws ni zipi au tayari umeshazijuwa na hivyo unajaribu kuzikimbia? Tusiwe wakubwa wa nadharia kusahau real applications. Hebu niambie hao watu waliostaarabika wote duniani wanafikia wapi mwisho wa relations zao, si celebrities, si royals , si viongozi ambao walio huru kuwa na uhusiano huo unaoueleza wewe.
Unaiaminisha jamii nzima.
Take ndoa for example. Ndoa ni kitu so central katika jamii kiasi cha kwamba ninavyokuja hapa kui-deconstruct watu wengine wanapata pause. Wanasema Astaghafirullah huyu Kiranga.
Lakini ukiangalia ninayoyasema yana ukweli. Ndoa ni stage ambayo katika utamaduni wetu wote tunategemewa kupita, ukishafikisha thirties tu watu wanaanza kukuzonga, harusi lini, wifi yetu yuko wapi, tunataka mjukuu etc.
Lakini ndoa yenyewe kiswahili mwanamme anaoa, mwanamke anaolewa.Na kiswahili hata kama mwanamke kachoka anataka kujitoa, hawezi kum divorce mume, inabidi amuombe mume amdivorce yeye mke.
Huo ndio mfumodume, umekaa katikati ya jamii yetu hata tunaposema "anaoa" na "anaolewa" hatujui kwamba ni mfumodume.
kwa hiyo, unamwaminisha nani? Jamii nzima. Unaiaminisha jamii kwamba mwanamme ni bora katika nini? Practiocally mambo yote ukiondoa mambo ya kike kama urembo, kuzaa, kulea watoto, kupika, umbea na mengine "ya kike kike" kama hayo.
Kwani nani anamsifia mwanaume kwa umalaya?
not to derail the original topic.
My sense is, huyu mama kauliza swali lililo so central katika kupata a paradigm shift katika jamii yetu.
Kwa nini tunakuwa so obsessed over sexual chastity kabla ya ceremony ya harusi/ndoa halafu tukishaihalalisha kwa misherehe inakuwa si big deal?
Watu wazima wawili wakipendana kwa kweli, what's the big deal about misherehe na other farcical extravagances?
Kiranga nimekuelewa,kuhusu neno "kuoa" au "kuolewa" wewe unalitafsiri vipi?Kuhusu mwanamke kutokuacha nafikiri hiyo inatokana na imani fulani,sidhani kama tunaweza lizungumzia hapa.Hayo maneno ya kiswahili bado sijaona ubaya wake,tatizo tunayachukulia kutokana na dhana ya mwanamke kutokutoa talaka ambayo kama nilivyosema ni dhana ya imani fulani tena moja tu.Kwenye mfumo dume hapo napo kuna mkanganyiko.Mwanaume na mambo ya kiume.Mwanamke na mambo ya kike.Tukubali kuwa mwanamke anapoambiwa "acha kufanya mambo ya kiume" ni sifa?Sidhani,pia mwanaume anapoambiwa acha mambo ya kike,sio aibu.Unapoyataja mambo ya kikekike wewe ndie unaamua yawe tusi,kashfa au vinginevyo.Tafsiri iliyoko kichwani mwako.Lakini pia huu mfumo unaoitwa dume una mambo mengi lakini mengi zaidi yapo vichwani mwetu zaidi,sio halisi!
Unaendeleza mfumodume.
Mie nakuuliza kwa nini unafikiri huyu dada, mwanamke, anataka kuolewa.
Wewe unaniuliza mwanamme kamchumbia kwa nini? Unampa prominence mwanamme, mtu ambaye hata sijamuulizia hapa. Mwanamke anaweza kuwa katika mahusiano na mwanamke, akitaka kumuoa huyo mwanamke, na mwanamke asiwe na haja ya kuolewa.
Zaidi ya hapo, neno "mchumba" hutumika loosely katika kiswahili kwa kumaanisha "boyfriend/girlfriend" na pia "fiancee" kwa sababu hatuna utamaduni wa boyfriend/girlfriend, ni mgeni. Sina hakika katika hii thread neno hili limetumika kama boyfriend au fiancee.
Kwa nini unamleta mwanamme katika swali lililomlenga mwanamke?
Kiranga kumbe tatizo ni michango ya Harusi? Jee iwapo hakuna michango jee hakuna tatizo?
Hebu kwa muwazi ,nini tatizo lako ndowa au mambo yanayofanywa kabla ya ndowa?
Tumekuwa tkihangaishana bure kumbe hukufahamu maudhui yangu! Labda niweke wazi zaidi.
Kwanini katika mara nyingi wazee wanawake wanawasaidia watoto wao na uhusiano wa nje ya ndowa? Na kwanini sisi wanaume huwa tunapinga mabinti wetu kuwa na uhusiano wa nje ya ndowa wakati tunajigharimukatika ndowa za wenetu ili uhusiano uwe ndani ya ndowa?