Mama huyu anahitaji msaada wenu!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951



Mama huyu pichani Rose Musoma anasumbuliwa na Ulemavu wa Viungo. Alipata ajali Wilayani Bukombe Mwaka 2008. Sasa yupo Mbagala Kingugi - Dar Es Salaam akiwa amepooza viungo na hajiwezi kwa kila jambo anatumia mfuko wa kutolea haja Ndogo. Anasumbuliwa na vidonda kutokana na kulala tu zaidi ya miaka minne (tokea 2008).Hawezi kukaa wala kusimama.

Taarifa ya ugonjwa wake imerushwa na TBC-1 Katika Kipindi cha "Wape Nafasi" leo tarehe 28.12.2012.

Kwa sasa anaishi na Mdogo wake Grace MUsoma aliyeolewa na hana uwezo wowote wa kumudu matibabu yake.

Alikimbiwa na mumewe baada ya kupata hiyo ajali. Ana watoto wawili wa Kike mmoja bado yupo Chekechea (huyo alienae pichani)

Shime wenye kuguswa na hali yake tushirikiane kumsaidia na Mungu atabariki kazi ya mikono yenu.

Anapatikana kwa simu 0769 358053 (hii ndio namba iliyorushwa na TBC 1)

Mbarikiwe wenye kujitoa.
 

Attachments

  • mama3.jpg
    52.9 KB · Views: 59
  • MAMA MSAADA -1.jpg
    75.6 KB · Views: 196
  • MAMA 2.jpg
    74.4 KB · Views: 53
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…