Kama kawaida najua kuna wale wanaojifanya much know wenye viherehere vya kutoa comments hata ambazo hazihusiani na mada yenyewe ambao hawataacha kutupia mitusi yao hapa. Ruksa kwa raha zako!!!
Ktk pitapita yangu nikakutana na hawa jamaa. Duuuu majina yanavyotamkwa huwezi fikiri ndio lile ulilozoea kusikia. Mfano: George tumezoea kutamka Joji wao ni Kyorkii, Gerard utasikia Kerari, Gilbert utasikia Keparti, imaculatha utasikia Makuna, Iluminate utasikia Mnate, Jacob au Yakobo Yakub utasikia Akupu nk. Huko Arusha nilikutana na jamaa tafsiri ya jina lake ni "radi" NAIKULUKULO. Ilinipa shida mwanzoni kulitamka. Ongeza na la kwako tucheke wote basi