Maisha yakiwa magumu

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,709
Reaction score
23,149
Hali ya ki uchumi kuanzia ngazi ya familia na mtu mmoja mmoja hapa nchini imekuwa mbaya sana.

Kwa mtu muoga wa maisha ambae rahisi kukumbwa na msongo wa mawazo/stress mpaka kufikia 2025 tunaweza kumkosa i mean kufa au kuwa mwehu so nimeona niwasihi waTz wenzangu kuhusu hii hali namna gani ya kukabiliana nayo.

1.Tambua hii hali si ya kwako peke yako(usije ukahisi kuwa wewe ndo mtu pekee unaecharazwa fimbo na haya maisha magumu Kwa kuwaza hivi itakusaidia kujipa moyo kuwa huu ni msiba wa wote na sio wako peke yako hivyo utajikuta umepata nguvu ya kusonga mbele.

2.Jiweke bize hata kama kwa shughuli ndogo ndogo kukukip bize au za kazini kwako la sivyo ubongo wako utakuwa bize kutafsiri mambo yote yaliyogoma kwenda na kukuogopesha kupiga hatua ya kupana na hali.

3.Punguza matumizi yasiyo ya lazima hapa namanisha utakachokipata hakikisha unakielekeza kwenye kununua vya msingi kwanza(basic need) then vije vya ziada.

4.Epuka kujihusisha sana na malalamiko juu ya serikali hii kwa sababu kulalamika sana kunaua juhudi za kupambana na hali uliyonayo.Muda wa kulalamika utumie kwenye kutafuta suluhisho ya matatizo yako.

5.Jikite kwenye kuishi kifamilia zaidi hapa namanisha achana na michepuko,kila unachokipata kiwe kinalenga kustawisha furaha ya familia kwa sababu familia ikiwa na furaha itakupa nguvu ya kupambana zaidi

6.ONGEZEA KWA MANUFAA YA UMMA.

NB:YATAISHA TU NI SWALA LA MUDA
Hashtag kwa Vyeti feki,wafanyabiashara,watumishi wote serikalini na private,wazee wastafu,vyama pinzani,walifukuzwa kazi kwa sababu mbalimbali.

NAOMBA KUWASILISHA
 
ili bandiko nasoma huku nimetoka mihangaiko yangu. kusema kweli imenipa moyo. nilipanga kesho nichelewe kwenda kwenye mihangaiko kwasababu leo mambo yalikua magumu. ila kesho saa11 nipo macho. Asante sana.
 
Naomba kila mtu asome namba 4 mara tatu itawasaidia kupunguza mawazo.
Ujumbe mzuri.
Alamsiki.
Kwaiyo unataka wapuuzi wakifanya upuuzi wao wote tushangilie........ La hasha, kuna wengine tumejaliwa upeo mpana wa kuona mambo lazima tuseme.......... Yaan kwa hali nchi ilipofika hata angepewa mtoto wa darasa la saba kuiendesha hii nchi wala asingeifikisha hapa.....
 
ili bandiko nasoma huku nimetoka mihangaiko yangu. kusema kweli imenipa moyo. nilipanga kesho nichelewe kwenda kwenye mihangaiko kwasababu leo mambo yalikua magumu. ila kesho saa11 nipo macho. Asante sana.
Mungu akutie nguvu hakuna kukata tamaa kwa sababu tukisusa kupambana tutazidi kuongeza matatizo zaidi.
 
Big up mkuu

Naongea kitu kimoja KUSHIRIKIANA -huwezi kufanikiwa peke yako,unahitaji kuwa na ushirikiano na watu sahihi,hutakiwi kuwa kisiwa,kuwa karibu shirikiana na watu positive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…