Mahaba Niue

Kipilipili

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2010
Posts
2,272
Reaction score
1,899
Ewe mahaba niue, kwake usinifufue.
Siniache nipumue, pumzi uzichukue.
Ewe mahaba nitwae,kwake moyoni nitue.
Mahaba sinizingue, niache nijizimue.

Mahaba nteketeze,niradhi kuangamia.
Mahaba n'nyong'onyeze,na nguvu kuniishia.
Mahaba nchombeze,nshindwe kujitambua.
Mahaba unipumbaze,kushinda hata bamia!

Ewe mahaba nifunge,"segerea" nsitoke!
Kwenye kinu unitwangwe,mashudu yaniondoke.
Ewe mahaba nipunge,kilingeni uniweke.
"Mama Ngina" sinitenge, tanifanya nteseke.

TABARUKU:kwa "mama Ngina" wangu na kwa WOTE walioko kwenye ndoa
NB: neno "Mama Ngina" limetumika kisanii tu ila halihusiane na mama ngina wa Jf au yeyote yule anaetumia jina hilo
 
Ewe mahaba niue, kwake usinifufue.
.........TABARUKU:kwa "mama Ngina" wangu na kwa WOTE walioko kwenye ndoa za halali!
......
Pole inaonyesha umezidiwa kete! Tunakuombea kwa aliye juu ili isifike hapa (BOFYA).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…