Madini kuipaisha Ruangwa

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555


KUTOKANA na kukua kwa kasi kwa shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, sekta hiyo inatarajiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kutoa kiasi kikubwa cha mapato wilayani humo, ikilinganishwa na sekta nyingine.

Kwa sasa halmashauri hiyo inapata mapato makubwa kupitia sekta ya kilimo kupitia mazao ya korosho, ufuta na mbaazi ambayo yanachangia asilimia 75 ya mapato yote. Msimu wa mwaka huu wilayani Ruangwa, korosho ziliingiza Sh bilioni 51, kati ya hizo Sh bilioni 36 zilikwenda moja kwa moja kwa wananchi, ufuta uliingiza Sh milioni 650, mbaazi Sh milioni 475 na misitu iliingiza Sh milioni 110.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Rashid Nakumbya wakati akizungumza na timu ya waandishi wa habari ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo mkoani Lindi kwa ajili ya maandalizi ya Jukwaa la Fursa za Uwekezaji na Biashara Lindi, linalotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 25 hadi 27, mwaka huu. Jukwaa hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 350, pia litafunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Kassin Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa mkoani humo.

Alisema kwa sasa Ruangwa imebainika kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya kila aina ikiwemo madini ya viwandani ya grafaiti na dhahabu ambayo tayari migodi imeanza uchimbaji. “Tuna kampuni tano za uchumbaji zinakaribia kuanza uchimbaji wa madini ya grafaiti na utati. Madini hayo ni muhimu sana katika sekta ya viwanda kwani yanatumika kutengenezea injini za ndege, betri za magari na saa lakini pia yanatumika kutengeneza kalamu,” alieleza.

Alisema kati ya kampuni hizo, iko kampuni kubwa ya Namungo Gemeni Gold Mine iliyopo eneo la Namungo inayoendela na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu huku kukiwa na wachimbaji wadogo wengi nao wakichimba madini hayo.

Nakumbya alisema madini hasa yalianza kujulikana wilayani humo mwaka 1999 hali iliyosababisha maendeleo ya halmashauri hiyo kubadilika ghaa na sasa kuna wenyeji wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakijishughulikisha na uchimbaji na shughuli nyingine za biashara.

Alisema pamoja na kwamba bado faida kubwa ya madini kama mapato haijaanza kuonekana kwa sasa, ila tayari dalili zinaonesha kuwa mchango wa madini hayo utakuwa mkubwa zaidi. Alieleza kuwa hali hiyo imeanza kuonekana kutokana na madini hayo kuanza kuchangia mapema katika shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa hoteli na nyumba za kisasa za wageni, nyumba za starehe lakini pia kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha.
 
Walikusanya kiasi gani ilipotoka green garnet zilizokuwa bora duniani
 
Mkutano utafanyikia Lindi mkoani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkutano utafanyikia Lindi mkoani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…