Madikteta waanza Kumkimbia Rais Putin, Duterte amkosoa vikali kuhusu uvamizi wa Ukraine

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,172
Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani, Rodrigo Duterte amemkosoa vikali Putin kwa mauaji ya raia wasiyo na hatia huku yeye akisema anauwa wahalifu.

Dikteita Duterte kumkosoa Putin ni ishara mbaya sana kwa Putin kutokana na Uvamizi wake nchini Ukraine, kwani inaonekana kitendo hicho hakikubaliki hata kwa baadhi ya madikteita wenzake.

________________________________________


Duterte amkosoa Putin kuhusu uvamizi nchini Ukraine

Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani Rodrigo Duterte, amemkosoa vikali kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kwa mauaji ya raia wasio na hatia nchini Ukraine, akisema wakati wote wawili wakitajwa kuwa wauaji, yeye anauwa wahalifu na wala sio watoto na wazee.

Duterte, ambaye amemwita wazi Putin kuwa rafiki, kwa mara ya kwanza, amekemea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wakati wa mkutano wa kila wiki na maafisa wakuu wa baraza la mawaziri unaopeperushwa kupitia televisheni ambapo alilaumu vita hivyo ambavyo vimedumu kwa miezi mitatu kwa kupanda kwa bei ya mafuta duniani ambako kumeathiri nchi nyingi, ikiwemo Ufilipino.

Huku akisisitiza kuwa hamlaani rais huyo wa Urusi, Duterte hakubaliani na kauli ya Putin ya uvamizi huo kuwa operesheni maalum ya kijeshi na kusema ni vita kamili vilivyoanzishwa dhidi ya taifa huru.

Chanzo DW

 
fungua tu uzi kila siku huko ni mwendo wa Dozi kwenda mbele ?
 
Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti,umesoma ila hujaelewa mantiki ya Duterte
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…