Kwanza niwapongeze sana madaktari wetu kwa ufanyajI wao wa kazi. Tanzania ni moja ya nchi ambayo madaktari wana status kubwa sana katika jamii japo hii imepungua kwa kipind hiki kutokana na wimbi kubwa la wanasiasa nchini.
Nimefanikiwa kufika hospitali tofauti nchini tatizo kubwa madaktari wetu hawataki kuongeleshwa lugha ya kidaktari. Ukitumia lugha ya kidaktari wanakukosoa vibaya mno as if unawafundisha kazi.
Madaktari wengi wanaposikia mgonjwa akitumia maneno kwa mfano femoral region(watu wa lugha mtanisaidia hapa) popliteal fossa au kutaja magonjwa ambayo unaona yanaweza kuwa yanakusumbua wanakosoa sana badala ya kutupa ufafanuzi.
Leo nimempeleka mdogo wangu hospital ana maumivu kwenye wrist joint nikafanya kauchunguzi kwanza kuhusu wrist joint na carpel tunnel kutokana na kashule nilikonako yaan kuvigusia tuu kwa daktari anakasirika as if nimemtusi .
Madaktari mtusikilize jaman na kutupa shule ikiwezekana .
Mtazamo nawasilisha..