Mabadiliko ni sasa, Iramba Magharibi

Wakati ni huu kamanda Mungu akusimamie na kwa kuwa unampango mwema wa kuwakomboa wanyonge lazima utafanikiwa ukimshirikisha Mungu. CCM lazima wapotee.
 
Hongera kaka,nani ataenda kumtoa janga la mkalama Salome mwambu,tunasubri kwa hamu ukombozi mkalama.
 

Kila la heri ila namba 4 naona haijakaa vyema usije ukaitwa msaliti.
 
Kila mtu anatamani kuwa mbunge.Hii ni baada ya kundi kubwa la wahuni kupitia chama kimoja cha upinzani kuwapeleka bungeni.
 
tunakwenda na jeska kishoa,iramba hatuwezi kuwakilishwa na mnyaturu.

Acha ukabila hayo mawazo yalishapitwa na wakati acha kuwakatisha tamaa vijana kwahiyo kishoa asipopitishwa utachagua ccm
 
Kila mtu anatamani kuwa mbunge.Hii ni baada ya kundi kubwa la wahuni kupitia chama kimoja cha upinzani kuwapeleka bungeni.

Naombea sana Diamond asioteshwe juu ya ubunge mwaka huu maana akigombea Kawe usijeshangaa kabisa Diamond akamuangusha Halima Mdee kwa kishindo.

Ubunge uliishapoteza maana.
 
Utakuwa msindikizaji tu
......mpe live!!!!!!

kila la heri
......yeah, kusindikiza sio, afike salama

Ccm itadumu daima madarakani
......ni kweli sasa kwa mtindo wa LONGOI CCM iachie nini kudumu? Tutaidumisha tu!!!

Japo mie sio CCM lakini Mwigulu Anatosha
......tena sana, natumia nafasi hii pia kumshauri Kilimba, aache siasa zake za maji taka, wakati wake umepita, IRAMBA haifanyi makosa tena kuchagua wacheza ngoma!!!!!
 
Sana kamanda. Hakuka hivi viatu vinakufaa. Ni watu kama nyie wenye uthubutu watakaoleta ukombozi wa Kweli Iramba.Tuko nyuma yako kaka. Tunahitaji vijana km wewe wa kuikomboa nchi hii. Utasimama, utatetea na kushindaaaa. Godluck bro.
 
"Whatever there be of progress in life
comes not through adaptation but
through daring."
Asanteni wana jamvi, japo safari ya ukombozi ni ndefu, HAKIKA bila kuthubutu, hatutopiga hatua yoyote mbele. Nitaanza mimi leo, lakini bila wana.Iramba kukipokea kijiti hiki cha mabadiliko, safari haitofika mwisho. Tushikamane, tutembee pamoja, tufike safari ya madiliko salama. With strong faith, hakika, TUTAFIKA.
 

Wee longoi ndugu yangu, na watia nia wengine Iramba, mnaonaje kama mkijipanga vizuri na kushika kata za kutisha ili wapatikane ma diwani wa kutosha, kuliko kurundikana ktk kugombea ubunge, mafanikio ni process, maendeleo ni gradual process.

Wakati wenzenu wakipambana kujenga chama, nyie mlificha, na mkawa wanafiki kwa kujenga makundi yasiyo na tija.

Wakati wa chaguzi za SM hakukuwa na longoi, kilimba wala jesca kukisaidia CDM kupata ushindi. Hembu tuwe wazalendo na wapenda maendeleo kweli.

Vijana walio pambana kuijenga CDM Iramba 90% wanagombea udiwani kwa sababu ni makamanda kweli na wanajua kuwa wana iramba wanahitaji baraza zuri na imara litakalo rudisha umiliki wa halmashauri kwa wananchi.

Longoi na wenzako, nawashauri mjishauri upya, na mpite mtaani mkijenge chama. Angalau nampongeza Jesca kajaribu kuvuna wanachama, tujenge chama huko vjjn kwanza, ndio turudi kutangaza nia.

pipoooooooozzzzz
 
Kaka, hmjui vizuri Longoi, wkt wa serikali za mitaa ni hasan pekee ndiye aliyewasaidia wagombea wa cdm kampeni na kutengeneza mihuri vijji vingi kama vile Ndulungu,nsonga,mgungia,misuna,mbelekese, urugu,ujungu,kisonga, msai,tyeme,shelui,ulemo,kyengege etc amefika wakati wa kampeni na alikuwa wakala kitongoji cha kilambazi-misuna ,hawa unaowataja tumewasikia jana tu.
 

Wee mfariji tu mwenzako badala ya kumpasha ukweli ili mapungufu ayafanyie kazi, unazidi kutudanganya. Iramba ni pana zaidi ya ufukiriavyo, kuwa mbunge ni zaidi ya kugawa mihuri.

Una habari kuwa huko kote alikogawa mihuri ya chama wanamtambua mgombea mwingine?

Ni nani ataaminiwa na wanachama kwa mitazamo ya haraka kati ya aliyegawa mihuri na yule aliyeenda kuzundua matawi hayo, kusimika bendera, kutoa kadi, kupokea wanachama wapya, n.k.

Longoi, huu mchakato sii wa ki lelemama. usifarijike kwa maneno kama "komaa utashinda ", . Utabaki kuwa msindikizaji kama wadau wengine walivyokwambia.

Wee njoo mtaani, piga mikutano ya kata, vuna wanachama watakao kupa ridhaa ya kugombea. Kamanda wa vita hakai nyumbani.

kila la kheri.
 
Unaona akili za maccm 'ccm itatawala milele- so what??? Nyambafu usilishushie heshima jimbo letu. Go longoi go.tutaamua sisi wananchi wa iramba nyie maccm msitupangie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…