fellinjohn7
Member
- Mar 15, 2013
- 65
- 39
Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendohata upendo wa Kimungu.
Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mumewangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia.
Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamuna urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usioelekea kabisa ngono na hata umoja wa kina au ibada ya upendo wa kidini.
Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamuna, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhuiyanayopatikana sana katika sanaa.
UFAFANUZI:
Neno la Kiingereza "love" linaweza kuwa na maana tofauti, lakini zinazohusiana, katika miktadha tofauti. Mara nyingi, lugha nyingine hutumia maneno mbalimbali kueleza dhanatofauti ambazo Kiingereza hutumia neno "love" kurejelea; mfano mmoja ni wingi wa maneno ya Kigiriki yanayorejelea "mapendo". Tofauti za utamaduni katika kufafanua mapenzi hivyo, hufanya liwe jambo gumu kuanzisha ufafanuzi wowote.
Ingawa desturi au chanzo cha mapenzi ni suala ambalo hujadiliwa mara kwa mara, sura tofauti ya neno hili zinaweza kuwekwa wazi kwa kuamua nini si mapenzi.
Kama njia ya kawaida ya kuonyesha hisia chanya (aina kubwa ya kupenda), mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na chuki (au kutojali); kama pendo ambalo linaegemea zaidi kwenye uhusiano wa kirafiki kuliko wa kingono, mapenzi kwa kawaida hugonganishwa na tamaa; na kama uhusiano kati ya watu, unaohusisha mahaba, mapenzi hugonganishwa na urafiki, ingawa neno mapenzi linaweza kutumika pia kwa urafiki wa karibu katika miktadha fulanifulani.
Wakati yanapojadiliwa kidhahania, mapenzikwa kawaida yanarejelea pendo kati ya watu, hisia alizonazo mtu kuhusu mtu mwingine. Mapenzi mara nyingi yanahusisha kutunza au kujiainisha na mtu au kitu, ikiwa ni pamoja na nafsi ya mtu.
Aidha, katika tofauti za kiutamaduni katika kuelewa mapenzi, mawazo kuhusu mapenzi pia yamebadilika sana kadiri ya wakati. Baadhi ya wanahistoria wanahusisha dhana za kisasa za mapenzi ya kimahaba na Ulayawakati au baada ya Karne za Kati, ingawa kuwepo kwa mahusiano ya kimahaba kabla ya wakati huo kunaonyeshwa na ushairi wa kimapenzi wa kale.
Kutokana na utata wa dhahania ya mapenzi, mjadala juu ya mapenzi kwa kawaida hupunguzwa hadi maneno yaliyopitwa na wakati, na kuna mithali kadhaa kuhusu mapenzi, mojawapo ikiwa ile ya Vergilio ya kuwa "Pendo hushinda yote" na ile ya Beatles"All you need is love" (Unachohitaji ni mapenzi tu).
Mwanafalsafa Gottfried Leibniz alisema mapenzi ni "kuwa na furaha tele kutokana na furaha ya mwingine."
Bertrand Russell anaelezea mapenzi kama hali ya "thamani kamili", kinyume na thamani inayobadilika.
MAPENZI YASIYOHUSISHWA NA MTU MAALAUM:
Mtu anaweza kusema anapenda nchi, kanuniau shabaha maalumu ikiwa anaithamini sana na kuizingatia kwa makini.
Vilevile, katika huduma za huruma na kazi za kujitolea "upendo" wa kazi unaweza kutokana na mapenzi yasiyohusishwa na kitu pamoja na utu na imani za kisiasa badala ya mapenzi kati ya watu.
Watu pia wanaweza "kupenda" vitu, wanyama, au shughuli ikiwa wao wenyewe watajitolea kujihusisha na vitu vile. Ikiwa tamaa ya kingono pia inashirikishwa, hali hii inaitwa parafilia.
Imeandaliwa na Wikipedia na kuchambuliwa na,
Senior John
0657035695