Mwanaspoti wanaweza wasiwe sahihi kwenye uteuzi wao kwa sababu zilizotajwa. Lakini sisi wananchi ndio wenye kasoro zaidi kwa kutuma sms bila ya kuhoji hayo mwanzoni, na tulioona hayo yakifanyika bila ya kutuma sms wala kuikosoa Mwanaspoti mpaka baada ya uteuzi. Tafsiri ya karibu ni kwamba tuliziona kasoro hizo, lakini tukajiingiza kutuma sms kwa imani kwamba wachezaji tuliowapenda ndio wangeshinda; sasa hawakushinda ndio tunalalamika. Tulipaswa kuhoji vigezo kwanza kabla ya kushiriki kupiga kura.