London student demonstration sees arrests and scuffles

TUJITEGEMEE

Platinum Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
27,581
Reaction score
28,612
Source:BBC

http://www.bbc.com/news/education-30113313

MY TAKE:

Wanafunzi wa Kitanzania hawana tena uwezo wa KUPINGA waziwazi maamuzi yanayofanywa na vyombo vya maamuzi yakilenga kuwanyanyasa,kuwadhalilisha,kuwakandamiza, na kuwadhulumu haki yao ya msingi ya kupata elimu. Wale wazamani kidogo walikuwa wanaweza.
 
Wanafunzi wa Kitanzania hawana tena uwezo wa KUPINGA waziwazi maamuzi yanayofanywa na vyombo vya maamuzi yakilenga kuwanyanyasa,kuwadhalilisha,kuwakandamiza, na kuwadhulumu haki yao ya msingi ya kupata elimu. Wale wazamani kidogo walikuwa wanaweza.

Marekani na Uingereza watoto wa mabilionea wazawa huwa wanalipa ada ndogo mno kwenye vyuo kuliko wanafunzi wa kitanzania.Mfano ukisoma chuo kimoja na mtoto wa Bilionea bill gates ada unayolipa mtoto wa kitanzania yaweza kuwa mara nne ya huyo wa bill gates.

Chuo hicho hicho kozi hiyo hiyo. Hebu nenda basi mkaandamane Uingereza na marekani kuwa hicho wanachofanya wanafunzi wa kitanzania si haki uone kama uwezo huo wa kuandamana marekani au uingereza upo au haupo.Kajaribuni.
 
......Hebu nenda basi mkaandamane Uingereza na marekani kuwa hicho wanachofanya wanafunzi wa kitanzania si haki uone kama uwezo huo wa kuandamana marekani au uingereza upo au haupo.Kajaribuni.
Mkuu sijakuelewa kabisa hapa una maanisha nini!?
 
Mkuu sijakuelewa kabisa hapa una maanisha nini!?

Ninamaanisha hivi nchi za kiafrika ni nchi maskini mno.Na vyuo vikuu vya Uingereza na marekani wanajua hilo.Sasa kwa nini wana mifumo ya ada miwili ambako mfano ada ya chuo kikuu Kwa mzawa ni dola 8000 wa Tanzania atachajiwa dola 24000 kwa kozi ile ile chuo hicho hicho.

Mwanafunzi maskini kutoka Tanzania hata akienda Uingereza au marekani lazima atalipa ada kubwa kuliko watoto matajiri wa kule.Ndio nikasema kama mnasema kuna uhuru wa kuandamana basi wanafunzi wa kitanzania nao waandamane kupinga huo ubaguzi Uliopindukia kwenye ada vyuo vya uingereza na marekani.
 
......Ndio nikasema kama mnasema kuna uhuru wa kuandamana basi wanafunzi wa kitanzania nao waandamane kupinga huo ubaguzi Uliopindukia kwenye ada vyuo vya uingereza na marekani.
Hapa sasa tupo pamoja, nadhani waafrica hawa walioko huko hawawezi kufanya hivyo si kwa kuogopa kupigwa na polisi kisha kuswekwa ndani bali kwa kuogopa wafadhili wao. Asilimia kubwa ya wanafunzi walioko huko wanafadhiliwa na mashirika na nchi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…