Leopard tours orders Tanzanian government

Duuh.., hadi Lowassa anapakatwa na huyu Fazal..! we Lowassa wewe..!
 
Mwaka mpya 2015 ulianza na kali ya mwaka baada ya ofisi ya serikali kuhamia kwa Zuher Fazal maarufu kama Fazal mmiliki wa LEOPARD TOURS.

Hili lilitokea baada ya mmiliki huyu kubuni njia yake batili ya kupunguza mishahara kwa 50% na kuwafukuza kazi wafanyakazi wake pasipo kuwalipa stahiki zao. Hii ni kutokana na kuyumba kwa biashara ya utalii nchi kupelekea mmiliki huyu kuyumba kiuchumi kutokana na kuendesha miradi mingi kwa wakati mmoja akitegemea kipato cha utalii nchini.

Mr. Fazal na RPC- Arusha waliwaundia zengwe (dili) wafanyakazi hao (SAFARI Guides) kuwa wamekuwa wakirudisha risiti zisizo halali ofisini (LEOPARD Tours).

Kutokana na kutokuja kwa watalii wanaoitembelea Tanzania kwa sababu ya hofu ya EBOLA AFRICA Mr. Fazal alimtumia RPC Arusha kwa manufaa yake binafsi kuwatisha wafanyakazi kwa kuwashinikiza wasaini kukubaliana ya kuwa walikuwa wakiibia kampuni (LEOPARD).

Pia twahisi dili (zengwe) hili pia atalitumia kukwepa au kupata punguzo la kodi kwa kisingizio alipata hasara, kifupi kajipanga. Twajiuliza kwa mwezi kweli itatokea Makumbusho ya Oldupai Gorge yaingize milioni mia nane(800milion)?

Hakuna idadi ya watalii kiasi hicho wanaopenda kutembelea mambo ya kale kupelekea kufikia pato 800milion kwa mwezi. Je inakuwaje yeye amekuwa akipata hasara ya 800milion kwa mwezi kwa miaka mitatu?

RPC Arusha alitumika vibaya kwa kuhamishia ofisi yake (ya umma) pamoja na polisi wake wakapewa Ofisi spesho ndani ya LEOPARD kwa ajili ya kucheza dili hili la kuwalazimisha wafanyakazi hao kusaini uongo.

Ilikuwa ni dili kwani ilikuwa ukikubaliana nao kuwa wewe ni mwizi hakuna shida upo free, ila kwa wale waliokataa gari ilikuwa tayari kuwapeleka Lock-up. Waliokataa walikaa lock-up zaidi ya siku nne hakuna dhamana wala kufunguliwa jalada lolote.

Baada ya kufanikisha alilokusudia tulilazimishwa ku-resign halafu kuomba kazi upya kwa kiwango cha mshahara atakaoamua(Barua za kuomba Kazi ni lazima kuandika). Mishahara yote ya nyuma(December) na Januari hii tutalipwa nusu mshahara na February kuendelea tutakatwa kiasi cha hela kwenye mishahara yetu kwa muda atakaoamua yeye mpaka hapo atakapofidia hasara yake ya million 800 kwa mwezi aliyokuwa akiipata kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita.

Mchakato huu mzima ulivyokuwa mpaka mwisho wa Igizo hili la Mr Fazal na huyu RPC Arusha hata mtoto mdogo ataelewa 'It was something planted'.

Yeye ameipakata serikali ya Tanzania ila ajue hajapakata " Facebook, Twitter na TripAdvisor". Waongoza watalii wote tupo kwenye mchakato wa kuliandika sakata hili kwa lugha zote za kigeni pamoja na unyanyasaji wote unaofanywa na LEOPARD TOURS.

Tutashea na waongoza utalii wote washee na marafiki(wazungu) wote tulio na mawasiliano nao na wao washee na marafiki zao huko ili wajue kusafiri kupitia kampuni hii siyo kumsaidia mtanzania bali ni kumkumbusha machungu ya mkoloni.

Muda si mrefu tutaambatanisha E-mail address wetu hapa ili waongoza watalii wote wanaopinga unyanyasaji mtutumie E-mail address za marafiki zenu (Watalii) mliokwisha safiri nao ili tushee nao huu unyanyasaji.

Twashukuru umoja ni nguvu!
 
KuaNguShA RoMa iLiChUKua MiAkA. BwaNa FaIzali NaOna yEye AtaAnGuKa vEry sOon nA kamPunI yake. KaMa waTu waTaenDelea kUtoA mAoVu Yake Nje. LeopArd imeFiKa diMiNishIng ratE oF reTurn. SAsa nI muDa wA kUfalll.
 
Kuhusu hao wanajeshi wa NEPAL,sio kweli kuwa Leopords Tours ni kampuni pekee iliyoajiri GHURKAs,nenda Migodini utakuta hao askari wa NEPAL wengi tu wameajiliwa kama security specialists,nenda kampuni kama G 4 security hao ndio wanaotumika kusindikiza hela,kwa hiyo ni udhaifu wa system kwani kama wanajeshi wastaafu wazuri tu si hata Tanzania wapo,ni kwanini serikali inaruhusu wanajeshi wastaafu wa Nepal walio serve jeshi la Uingereza wapate ajira za ulinzi katika nchi yenye wastaafu wengi hadi makomandoo ambao kwa mshahara wanaolipwa hao ma-ghurka wangekubali tu kuajiliwa na makampuni hayo.
 
Kwahiyo J.K nae amepakatwa na Fazal.., we J.K wewe.., najua we ni dhaifu..., ila kwa hili onyesha makucha bhana.., pliiiz.., usituaibishe bana..
 
bado hujatuelezea anavunjaje haki za binadam, muandishi umetoa nadharia ya kama mtu ambaye analazimishia leopard aonekane muovu. Anaweza kua kweli Muovu ila Muandishi maandika hayajajenga hoja ya kuridhisha zaidi ya kurudia tu kusema kua anawatesa wafanyakazi na kuminya haki za binadam.

Toa ufafanuzi mfano: Malipo ya mshahara ni kiasi usd 700 hivyo ni mategemeo yetu kua nssf inawekwa kiasi (say usd 50) ila cha ajabu tumegundua kua inayowekwa ni Usd 10.. kwa ufafanuzi huu wasomaji tunakua tumejionea wenyewe kosa la Uyo jamaa liko wapi. "pia lazima ieleweke kua kuna uwezekano unachochukulia kua ni mshahara si mshahara bali ni mshahara plus bonus .. hivyo rate ya nssf inakatwa kwenye mshahara tu na si bonus. watu wa H.R wanajua zaidi kuhusu.

Kwa bahati mbaya tunashindwa kusikia upande wa pili kujua kama hizi shutma zina ukweli wa kiasi gani. ili tukamhukumu kimtandao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…